Hii itakuwa muhimu kwa sababu kadhaa: Ingeifanya Tor iweze kushughulikia vizuri mpangilio mpya kama VoIP. Inaweza kutatua hitaji zima la programu kwa kutumia vyanzo mbambali. Exit relays pia haitahitaji kutenga maelezo mengi ya mafaili kwa muunganisho yote ya kutoka.

Tunaelekea upande huu. Baadhi ya matatizo magumu ni:

  1. Pakiti za IP zinaonesha sifa za OS. Bado tungehitaji kufanya marekebisho katika pakiti za kiwango cha IP, kwa kusimamisha mashambulizi kama TCP fingerprinting. Kwa kuzingatia utofauti na utata wa ukubwa wa TCP, pamoja na mashambulizi ya vifaa katika fingerprinting, inaonekana kama njia bora ya kubashiri ni kusafirisha mrundikano wetu wa nafasi ya mtumiaji katika TCP.

  2. Mtiririko wa kiwango cha programu bado unahitaji kupangwa ukamilike. Bado tunahitaji programu tumizi kwa upande wa mtumiaji kama vile Torbutton. Kwahiyo haitakuwa tu suala la kuzinasa pakiti na kuzificha katika tabaka la IP.

  3. Mpangilio fulani utaendelea kuvujisha taarifa. Kwa mfano, ni lazima tuandike upya maombi la DNS kwa hivyo huwasilishwa kwa seva ya DNS isiyoweza kuunganisha badala ya seva ya DNS katika mtoa huduma za watumiaji, hivyo, lazima tuelewe miongozo tunayoisafirisha.

  4. DTLS (datagram TLS) kimsingi hazina watumiaji, na IPsec kwa hakika ni kubwa. Mara tu tumechagua mfumo wa usafirishaji, tunahitaji kuunda mpangilio mpya wa end-to-end Tor kwa kuepuka mashambulizi ya kuweka alama na masuala mengine yanayoweza kujitokeza kutokujulikana kwa muda sasa tumeruhusu njia chache, kutuma upya , na kadhalika.

  5. Sera za kutoka kwa pakiti za kiholela za IP inamaanisha kutengeneza mfumo salama wa kutambua usimamizi usafirishwaji wa data (IDS). Waendeshaji wetu wa node hutuambia kuwa sera hizi za kutoka ni moja ya sababu kuu wapo tayari kutumia Tor. Kuongeza IDS ili kutunza sera za kutoka kutaongeza utata kwa usalama wa Tor, na hakutaweza kufanya kazi kivyovyote, kama inavyothibitisha na taaluma nzima ya IDS na karatasi za kukubaliana na IDS. Masuala mengi ya unyanyasaji yanaweza kutatuliwa na ukweli kwamba Tor husafirisha mtiririko halali wa TCP (kinyume na IP iliyopangiliwa kiholela ikijumuisha pakiti zisizotengenezwa na IP hatarishi.) Sera za kutoka zimekuwa za muhimu zaidi pale tunapokuwa tayari kusafirisha pakiti za IP. Pia tunahitaji maelezo ya ukamilifu ya sera za kutoka katika saraka ya Tor, hivyo watumiaji wanaweza kutabiri nodes zipi zitaruhusu pakiti zao kutoka. Watumiaji pia wanahitaji kutabiri pakiti zote ambazo watataka kuzituma kwa kipindi kabla ya kuchagua exit node yao!

  6. Nafasi za jina la Tor-internala zingehitaji kuundwa upya. Tunaunga mkono anwani za onion service ".onion" kwa kukatiza anwani zinapopitishwa kwa mtumiaji wa Tor. Kwa kufanya hivyo kiwango cha IP kutahitaji kuanzisha muunganisho mkubwa zaidi unaoonekana kati ya Tor na local DNS resolver.