Kama programu zako za ulinzi zinafanya kazi kwa kuzuia vifaa, unaweza kuiambia Tor kutumia vifaa pale tu unapoanza Tor Browser yako. Au unaweza kuongeza vifaa ambavyo programu zako za ulinzi inaruhusu kwa kuongeza"FascistFirewall 1" katika faili lako la kusanidi torrc. Katika asili yake, unapopangilia hii Tor huzani kwamba programu zako za ulinzi zinaruhusu tu port 80 na port 443 (HTTP na HTTPS kama inavyofuatana). Unaweza kuchagua seti tofauti ya vifaa katika machaguo ya FirewallPorts torrc . Ukitaka kuwa sawa pamoja na udhibiti wako, pia unaweza kutumia chaguo la kusanidi la ReachableAddresses, mfano.:

ReachableDirAddresses *:80
ReachableORAddresses *:443