Hakuna mlango wa nyuma kabisa katika Tor.
Tunajua baadhi wa wanasheria mahiri ambao husema kwamba haiwezekani mtu yeyote atajaribu kutufanya tuongeze kitu katika mamlaka yetu (Marekani).
Kama wangetuuliza, tutapambana nao, na (wanasheria wanasema)kunauwezekano wa kushinda.
Hatutoweka mlango wa nyuma kwenye Tor.
Tunafikiri kwamba kuweka mlango wa nyuma katika Tor unaweza kuwa uzembe wa uwajibikaji kwa watumiaji wetu, na mfano mbaya kwa usalama wa programu kwa ujumla.
Kama tukiweka mlango wa nyuma wa makusudi katika ulinzi wa programu yetu, itaharibu utaalamu wa hadhi yetu.
Hakuna mtu atakayeamini programu yetu tena- kwa sababu nzuri!
Kwa kusema hivyo, bado kuna mashambulizi mengi ambayo watu wanaweza wakajaribu.
Mtu mwingine anaweza kujimilikisha sisi, au kuingilia compyuta zetu, au kitu chochote kama hicho.
Tor ni chanzo huru, na kila mara unaweza kuangalia chanzo ( au angalau utofauti tangu toleo la mwisho) kwa vitu vya tuhuma.
Kama sisi ( wasambazaji ambao wamekupatia Tor) hawajakupa uwezo wa kuifikia msimbo wa chanzo, kuna uhakika kuwa kuna alama ya kitu cha kuchekesha kinaendelea.
Vilevile unatakiwa kuangalia Sahihis za PGP] katika matoleo, kuhakikisha hakuna aliye haribu na tovuti za msambazaji.
Pia, zinaweza kutokea ajali za bahati mbaya katika Tor ambazo zinaweza zikaathiri kutojulikana kwako.
Mara kwa mara huwa tunapata na kurekebisha hitilafu zinazohusiana na kutojulikana, hakikisha unasasisha toleo la Tor yako.