Tor Inaunganishwa

Moja ya masuala ya kawaida ambayo husababisha makosa ya unganisho kwenye Tor Broswer ni mfumo wa saa usio sahihi. Tafadhari hakikisha mfumo wa saa na majira zimewekwa kwa usahihi. Kama hii haitatui tatizo, angalia Troubleshooting page on the Tor Browser manual.

Kama unapata changamoto katika kuunganisha, ujumbe wa dosari unaweza kutokea na unaweza kiuchagua "copy Tor log to clipboard". Kisha nakili matatizo ya Tor log katika faili la kipimo au nyaraka nyingine.

Ikiwa hutaona chaguo na Tor Browser ikiwa inafanya kazi, unaweza kuingia katika hamburger menu ("≡"), halafu bonyeza "settings", na mwishoni "Connection" katika apande wa pembeni. Chini katika kurasa, pembeni ya maandishi ya "View the Tor logs", bofya kitufe cha "View Logs...".

Njia mbadala, katika GNU/Linux, kuona tatizo hapohapo katika kifaa, peruzi katika saraka ya Tor Browserna ianzishe kutumia Tor Browser kutoka katika sehemu ya amri:

./start-tor-browser.desktop --verbose

au kutunza kumbukumbu katika faili (default: tor-browser.log)

./start-tor-browser.desktop --log [file]

Utapaswa kuona mojawapo ya makosa katika kumbukumbu za kawaida (angalia mistari ifuatayo katika kumbukumbu zako za Tor):

Kumbukumbu ya hitilafu ya kawaida #1: Kushindwa kwa muunganiko wa Proxy

2017-10-29 09:23:40.800 [NOTICE] Opening Socks listener on 127.0.0.1:9150
2017-10-29 09:23:47.900 [NOTICE] Bootstrapped 5%: Connecting to directory server
2017-10-29 09:23:47.900 [NOTICE] Bootstrapped 10%: Finishing handshake with directory server
2017-10-29 09:24:08.900 [WARN] Proxy Client: unable to connect to xx..xxx..xxx.xx:xxxxx ("general SOCKS server failure")

Ikiwa utaona mistari kama hii katika kumbukumbu za Tor, hii inamaanisha zinashindwa kuunganishwa katika SOCKS proxy. Ikiwa SOCKS proxy itahitajika katika mapngilio wa mtandao wako, basi tafadhali hakikisha kuwa umeingiza maelezo yako katika proxy kwa usahihi. Ikiwa SOCKS proxy haihitajiki, au hauna uhakika, tafadhari jaribu kuunganisha mtandao wa Tor bila kutumia SOCKS proxy.

Kumbukumbu la kosa la kawaida #2. Haifikii guard relays

11/1/2017 21:11:43 PM.500 [NOTICE] Opening Socks listener on 127.0.0.1:9150
11/1/2017 21:11:44 PM.300 [NOTICE] Bootstrapped 80%: Connecting to the Tor network
11/1/2017 21:11:44 PM.300 [WARN] Failed to find node for hop 0 of our path. Discarding this circuit.
11/1/2017 21:11:44 PM.500 [NOTICE] Bootstrapped 85%: Finishing handshake with first hop
11/1/2017 21:11:45 PM.300 [WARN] Failed to find node for hop 0 of our path. Discarding this circuit.

Ikiwa utaona mistari kama hii katika kumbukumbu za Tor, hii inamanisha Tor imeshindwa kuunganisha node ya kwanza katika Tor circuit. Hii inaweza kumaanisha kuwa upo katika mtandao uliodhibitiwa.

Tafadhari jaribu kuunganisha kupitia bridges, na baada ya hapo inapaswa kurekebisha tatizo.

Kumbukumbu la kosa la kawaida #3; Imeshindwa kukamilisha TLS handshake

13-11-17 19:52:24.300 [NOTICE] Bootstrapped 10%: Finishing handshake with directory server 
13-11-17 19:53:49.300 [WARN] Problem bootstrapping. Stuck at 10%: Finishing handshake with directory server. (DONE; DONE; count 10; recommendation warn; host [host] at xxx.xxx.xxx.xx:xxx) 
13-11-17 19:53:49.300 [WARN] 10 connections have failed: 
13-11-17 19:53:49.300 [WARN]  9 connections died in state handshaking (TLS) with SSL state SSLv2/v3 read server hello A in HANDSHAKE 
13-11-17 19:53:49.300 [WARN]  1 connections died in state connect()ing with SSL state (No SSL object)

Ikiwa utaona mistari hii katika kumbukumbu za Tor, hii inamaanisha Tor imeshinda kumalizia TLS handshake katika directory. Kutumia madaraja inaweza kurekebisha hii.

Kumbukumbu la kosa la kawaida #4: Clock skew

19.11.2017 00:04:47.400 [NOTICE] Opening Socks listener on 127.0.0.1:9150 
19.11.2017 00:04:48.000 [NOTICE] Bootstrapped 5%: Connecting to directory server 
19.11.2017 00:04:48.200 [NOTICE] Bootstrapped 10%: Finishing handshake with directory server 
19.11.2017 00:04:48.800 [WARN] Received NETINFO cell with skewed time (OR:xxx.xx.x.xx:xxxx): It seems that our clock is behind by 1 days, 0 hours, 1 minutes, or that theirs is ahead. Tor requires an accurate clock to work: please check your time, timezone, and date settings.

Ikiwa utaona mistari hii katika kumbukumbu za Tor, hii inamaanisha mfumo wako wa saa haupo sahihi. Tafadhari hakikisha saa yako imewekwa sahihi, ikiwemo usahihi wa majira ya ukanda, Halafu anzisha tena Tor.

Makosa ya seva ya proxy yanaweza kutokea kwa sababu mbalimbali. Unaweza kujaribu shughuli zifuatazo mojawapo au zaidi pale tu unapohesabu makosa haya:

  • Ikiwa una programu za kuzuia programu hatarishi, inaweza ingilia huduma za Tor. Zima programu ya kuzuia programu hatarishi na anzisha tena browser.
  • Hupaswi kuhamisha folda la Tor Browser kutoka katika eneo halisi kwenda eneo tofauti. Ikiwa ulifanya hili, rudisha mabadiliko.
  • Unapaswa pia kuangalia sehemu inayounganisha mawasiliano kama umeiunganisha. Jaribu sehemu mbalimbali zinazounganisha kutoka kwa zinazotumika sasa, kama vile 9050 au 9150.
  • Wakati mwingine yote hushindikana, anzisha upya browser. Muda huu, mhakikisha kusanikisha Tor Browser katika saraka mpya, sio juu ya Browser iliyosanikishwa hapo awali.

Ikiwa kosa litaendelea, tafadhari wasiliana nasi.

Kama huwezi kuipata onion services unazo taka, hakikisha umeingiza onion address 56 kwa usahihi; hata makosa madogo itazuia Tor Browser ili uweze kuzifikia site. Kama bado una shindwa kujiunga na onion services, tafadhali jaribu tena baadaye. Inaweza kuwa na tatizo la muda mfupi la muunganiko, au wanaoendesha tovuti wanaweza kuwa wameruhusu kukatika kwa mtandao bila angalizo.

Pia unaweza kuhakikisha kuwa unaweza kuzipata onion services kwa kujiunga na onion services za DuckDuck.