Katika toleo la Tor Browser la 6.0.6, tulihamisha kwenda DuckDuckGo kama injini ya msingi ya utafutaji.
Kwa muda sasa, Tenganisha, ilikua inatumika kwenye Tor Browser, ilikua haiwezi kupata matokeo ya Google search.
Tangu Tenganisha ni zaidi ya utafutaji wa injini ya Meta, ambayo inaruhusu watumiaji kuchagua kati ya watoa huduma za utafutaji tofauti, itarudi nyuma kuleta matokeo ya utafutaji wa Bing, ambayo hayakukubalika ubora wake.
DuckDuckGo haingii, hukusanya au sambaza taarifa binafsi za mtumiaji au historia yao ya walivyotafuta, na hivyo ni nafasi bora kulinda faragha yako.
Injini nyingine nyingi za kuuliza vitu huifadhi ulivyovitafuta na taarifa nyingine kama vile muda uliotafuta, anwani yako ya IP na taarifa za akaunti yako kama uliingia.