Tor Browser

Digital signature ni mfumo unaohakikisha kua kifurushi fulani kilitolewa na watengenezaji na haikuharibiwa. Chini tunaelezea kwa nini ni muhimu na jinsi ya kuhakiki kuwa Tor Browser ulopakua ndio ile tulichotengeneza sisi na hakijabadilishwa na mtu anayeshambulia.

Kila faili katika ukurasa wetu wa kupakuainakuja na faili iliyo na lebo "saini" yenye jina sawa na kifurushi na kiambishi ".asc". Faili hizi zipo wazi na saini ya OpenPGP. Itakuruhusu kuthibitisha faili ulilo sasisha ambalo hasa tulilikusudia upate. Hii itatofuatiana kutokana na kivinjari, lakini kwa ujumla unaweza kupakua faili hili kwa kubofya kitufe cha kulia katika sehemu ya "signature"na kwa kuchagua chaguo la "save file as".

Kwa mfano, tor-browser-windows-x86_64-portable-13.0.1.exeinaambatanwa na tor-browser-windows-x86_64-portable-13.0.1.exe.asc. Kuna mfano jina la faili halifanani kabisa na jina la faili ulilopakua.

Kwa sasa tunaonesha ni kwa jinsi gani unaweza kuthibitisha faili lililopakuliwa kwa digital signature katika mifumo mbalimbali ya uendeshaji. Tafadhali kumbuka kuwa sahihi ni tarehe wakati kifurushi kimetiwa sahihi. Kwa ujumla kila muda faili jipya linapakuliwa kwa sahihi mpya inayotokana na tarehe tofauti. Ilimradi umeshathibitisha sahihi hupaswi kujali kuwa tarehe iliyoripotiwa inaweza kutofautiana.

pakua GnuPG

Awali ya yote unahitaji kuwa na GnuPG iliyosanidiwa kabla haujathibitisha sahihi.

Kwa watumiaji wa Windows:

Ikiwa unatumia windowa, pakua Gpg4win na endesha kisanikishi chake.

Ili kuthibitisha sahihi unahitaji kuandika commands chache katika mstari wa command wa window, cmd.exe.

Kwa watumiaji wa macOS:

Ikiwa unatumia macOS, unaweza sanikisha GPGTools.

Ili kuthibitisha sahihi unahitaji kuandika command chache katika Terminal (under "Applications").

Kwa watumiaji wa GNU/Linux:

Ikiwa unatumia GNU/Linux, labda tayari unayo GnuPG katika mfumo wako, kwa kuwa usambazaji mwingi wa GNU/Linux huja ikiwa imewekwa tayari.

Ili kuthibitisha saini, utahitaji kuingiza maagizo machache kwenye kompyuta. Jinsi ya kufanya hivyo itatofautiana kulingana na usambazaji wako.

kutafuta Tor kwa funguo ya watengenezaji

Timu ya Tor Browser imesaini Tor Browser ilioachiwa. Ingiza Tor Browser kwa watengeneza programu kusaini funguo (0xEF6E286DDA85EA2A4BA7DE684E2C6E8793298290):

gpg --auto-key-locate nodefault,wkd --locate-keys torbrowser@torproject.org

Hii inatakiwa kukuonyesha kitu fulani kama vile:

gpg: key 4E2C6E8793298290: public key "Tor Browser Developers (signing key) <torbrowser@torproject.org>" imported
gpg: Jumla ya number ya zilizoshughulikiwa: 1
gpg:        imported: 1
pub  rsa4096 2014-12-15 [C] [expires: 2025-07-21]
   EF6E286DDA85EA2A4BA7DE684E2C6E8793298290
uid      [ unknown] Tor Browser Developers (signing key) <torbrowser@torproject.org>
sub  rsa4096 2018-05-26 [S] [expires: 2020-12-19]

Ikiwa utapata ujumbe wa kosa, kitu kimeenda vibaya na huwezi kuendelea mpaka utambue kwa nini hii haikufanya kazi. Huenda ukaweza kuagiza ufunguo kwa kutumia sehemu ya Kuzunguka tatizo (kwa kutumia ufunguo wa umma) badala yake.

Baada ya kuingiza funguo, unapaswa kuzitunza katika faili (kiutambua kwa fingerprint hapa):

gpg --output ./tor.keyring --export 0xEF6E286DDA85EA2A4BA7DE684E2C6E8793298290

Matokeo ya amri ni muhimu kuhifadhiwa katika faili lililopatikana ./tor.keyring, mfano katika muongozo wa sasa. Kama ./or.keyring haipo baada ya kutumia command hii, kuna kitu kina makosa na huwezi kuendelea hadi uwe umetatua kwanini hichi hakifanyi kazi.

hakiki saini

Kuhakiki saini ya kifurushi ulichopakua, utahitaji kupakua saini ya ".asc" inayohusiana nayo pamoja na faili la kusakinisha lenyewe, na uihakiki kitufe kinachotaka GnuPG kuhakiki faili lililopakuliwa.

Mifano hapa chini inadhani kuwa ulipakua mafaili haya mawili kwenye folda lako la "Downloads". Kumbuka kuwa hizi amri hutumia mfano wa majina ya faili na yako itakuwa tofauti: unaweza kuhitaji kubadilisha majina ya faili za mfano na majina kamili ya faili ambazo umepakua.

Kwa watumiaji wa Windows(badili x86_64 hadi i686 ikiwa una vifurushi 32-bit):

gpgv --keyring .\tor.keyring Downloads\tor-browser-windows-x86_64-portable-13.0.1.exe.asc Downloads\tor-browser-windows-x86_64-portable-13.0.1.exe

Kwa watumiaji wa macOS:

gpgv --keyring ./tor.keyring ~/Downloads/tor-browser-macos-13.0.1.dmg.asc ~/Downloads/tor-browser-macos-13.0.1.dmg

Kwa watumiaji wa GNU/Linux (badili 6x86_64 hadi i686 ikiwa una vifurushi 32-bit):

gpgv --keyring ./tor.keyring ~/Downloads/tor-browser-linux-x86_64-13.0.1.tar.xz.asc ~/Downloads/tor-browser-linux-x86_64-13.0.1.tar.xz

Matokeo ya amri inapaswa kuwa ina:

gpgv: Good signature from "Tor Browser Developers (signing key) <torbrowser@torproject.org>"

Ikiwa unapata ujumbe wenye makosa zenye "No such file or directory', labda kuna kitu hakipo sawa katika hatua mojawapo zilizopita, au umesahau kuwa hizi command unazotumia kwa mfano majina ya file na yako yatakuwa na utofauti kidogo.

Inaonyesha upya kifunguo cha PGP

Endesha amri ifuatayo ili kuonyesha upya ufunguo wa kutia sahihi wa Wasanidi wa Kivinjari cha Tor katika uwekaji wa keyring kutoka kwa keyserver. Hii pia itachukua subkey mpya.

gpg --refresh-keys EF6E286DDA85EA2A4BA7DE684E2C6E8793298290

Njia mbadala kwa kutumia (funguo ya umma)

Kama unakutana na makosa unaweza rekebisha, kuwa huru kupakua na kutumia funguo ya umma badala. njia mbadala unaweza kutumia njia zifuatazo:

curl -s https://openpgpkey.torproject.org/.well-known/openpgpkey/torproject.org/hu/kounek7zrdx745qydx6p59t9mqjpuhdf |gpg --import -

Mtengenezaji wa alama maalum za utambuzi za Tor Browser pia anapatikana katikakeys.openpgp.org na kuiweza kupakuliowa kutoka https://keys.openpgp.org/vks/v1/by-fingerprint/EF6E286DDA85EA2A4BA7DE684E2C6E8793298290. Ikiwa unatumia MacOS au GNU/Linux, ufunguo unaweza kupatikana kwa kutumia njia ifuatayo:

gpg --keyserver keys.openpgp.org --search-keys EF6E286DDA85EA2A4BA7DE684E2C6E8793298290

unaweza pia kuhitaji kujifunza zaidi kuhusu GnuPG.

Faili ulilopakua na kulifanyiakazi inakuhimiza kwa marudio. Ikiwa haukumbuki,kuna uwzekano mkubwa folda lako kupakuliwa au Desktop.

Mpangilio chaguo-msingi katika kisakinishi cha Windows pia hukuundia njia ya mkato kwenye Desktop yako, ingawa fahamu kuwa huenda umeacha kuchagua kwa bahati mbaya chaguo la kuunda njia ya mkato.

Ikiwa hauwezi kuipata katika mojawapo ya folda hizo,pakua tena na angalia prompt ambayo imekuuliza kuchagua saraka ya kuipakua. Chagua eneo la moja kwa moja ambalo utakumbuka kwa urahisi, na mara upakuaji ukikamilika unapaswa kuona folda la Tor Browser.

Kila tunapotoa tolea jipya laf Tor Browser iliyo imara, tuaandika chapisho la blogi lenye maelezo kuhusiana nayo na vipengere na sifa mpya zilizopo na matatiozo yanayofahamika. Kama umeanza kupata matatizo katika Tor Browser yako baada ya kusasisha, angalia blog.torproject.org kwa ajili ya chapisho lihusulo Tor Browser imara ya hivi karibuni kuona kama tatizo lako limeorodheshwa. Kama tatizo lako halijaorodheshwa huko, tafadhali kwanza angalia Tor Browser's issue tracker na tengeneza GitLab issue kuhusiana na ulichokutana nacho.

Tunataka kila mtu aweze kufurahia Kivinjari cha Tor katika lugha yao wenyewe. Kivinjari cha Tor sasa kinapatikana katika lugha nyingi, na tunajitahidi kuongeza zaidi.

Orodha yetu mpya ya lugha saidizi ni:

Lugha
العربية (ar)
Català (ca)
česky (cs)
Dansk (da)
Deutsch (de)
Ελληνικά (el)
English (en)
Español (es)
ﻑﺍﺮﺴﯾ (fa)
Suomi (fi)
Français (fr)
Gaeilge (ga-IE)
עברית (he)
Magyar nyelv (hu)
Indonesia (id)
Islenska (is)
Italiano (it)
日本語 (ja)
ქართული (ka)
한국어 (ko)
lietuvių kalba (lt)
македонски (mk)
ﺐﻫﺎﺳ ﻡﻼﻳﻭ (ms)
မြမစ (my)
Norsk Bokmål (nb-NO)
Nederlands (nl)
Polszczyzna (pl)
Português Brasil(pt-BR)
Română (ro)
Русский (ru)
Shqip (sq)
Svenska (sv-SE)
ภาษาไทย (th)
Türkçe (tr)
Український (uk)
Tiếng Việt (vi)
简体中文 (zh-CN)
正體字 (zh-TW)

Unataka kutusaidia kutafsiri? Kuwa mtafsiri wa Tor!

Pia unaweza kutusaidia kupima lugha zinazofuata tutakazotoa, kwa kusakinisha na kupima toleo la Alpha la Tor Browser.

hapana, Tor Browser ni programu huria na ni bure. kivinjari chochote kinachokulazimisha kulipia na inadai kuwa Tor Browser ni feki. Ili kuhakikisha kuwa unapakua kivinjari sahihi cha Tor Browser tembelea ukurasa wetu wa kupakua kwa kubofya hapa:download page. Baada ya kupakua, unaweza kuhakikisha kuwa una toleo rasmi la Tor Browser kwa kuthibitisha saini. Kama unashindwa kufungua tovuti yetu. tembelea censorship section]kupata habari kuhusu njia mbadala ya kupakua Tor Browser.

Ikiwa umelipia programu ghushi inayodai kuwa Kivinjari cha Tor, unaweza kujaribu kuomba kurejeshewa pesa kutoka kwa Apple au Play Store au unaweza kuwasiliana na benki yako ili kuripoti shughuli ya ulaghai. Hatuwezi kukurejeshea pesa kwa ununuzi uliofanywa kwa kampuni nyingine.

Unaweza kutoa taarifa kwa Tor Browser feki kwenye frontdesk@torproject.org

Tor Browser kwa sasa inapatikana kwenye Windows, Linux, macOS na Android.

Kwenye Android, Mradi wa Guardian pia hutoa programu ya Orbot kuelekeza programu zingine kwenye kifaa chako cha Android kupitia mtandao wa Tor.

Hakuna toleo rasmi la Kivinjari cha Tor kwa iOS bado, kama ilivyoelezwa katika chapisho hili la blogu. Pendekezo letu bora linalopatikana ni Kivinjari cha Onion.

Kwa bahati mbaya, hatuna toleo la Tor Browser kwa ajili ya Chrome OS. Utaweza kutumia Tor Browser kwa Android kwenye Chrome OS. Zingatia kwa kutumia Tor ya simu kwenye Chrome OS, utaona toleo la simu la tovuti. Japokuwa, kwa sababu hatuchunguzwi kwenye app ya Chrome OS, hatujui kama vipengele vyote vya faragha vya Tor Browser kwa ajili ya watumiaji wa Android vitafanya kazi vizuri.

Samahani, lakini kwa sasa hakuna msaada rasmi wa kutumia Tor Browser katika *BSD. Kuna kitu kinaitwa TorBSD project, lakini Tor Browser haijawezeshwa rasmi.

Unapotumia Tor Browser wakati mwingine inaweza kuwa taratibu kuliko kivinjari kingine. Mtandao wa Tor una watumiaji wa kila siku zaidi ya milioni, na zaidi ya ralays 6000 kwa ajili ya kusafirisha data zoite, na mzigo katika kila seva unaweza kusababisha ucheleshwaji. Na, kwa muundo, usafirishaji wako unaruka kwa kupitia seva za wanajitolea katika vifaa mbalimbali duniani, na kwa kawaida baadhi ya vikwazo na ucheleshwaji utakuwepo. Unaweza kusaidia kuborewsha kasi ya mtandao kwa running your own relay, au kuhamasisha wengine kufanya hivyo. Kwa majibu ya kina zaidi, angaliaChapisho la blogu la Roger kuhusu mada na Mada za Tor's Open Research: toleo la 2018 kuhusu Utendaji wa Mtandao. Unaweza pia kuangalia chapisho letu la hivi majuzi la blogu Ulinzi wa mtandao wa Tor dhidi ya Mashambulizi Yanayoendelea, ambalo linajadili mashambulizi ya Kunyimwa Huduma (DoS) kwenye Tor Mtandao. Zaidi ya hayo, tumeanzisha Ulinzi wa Uthibitisho wa Kazi kwa Huduma za Onion ili kusaidia kupunguza baadhi ya mashambulizi haya. Kusema hivyo, Tor ni ya haraka zadi ya ilivyokuwa mwanzo na unaweza usigundue tofauti yoyote katika kasi ukilinganisha na vkivinjari kingine.

Huku majina yanaweza yakaashiria, 'muundo wa Incognito' na 'tab za faragha' haifanyi ujulikane kwenye mtandao. Wanaondoa taarifa zote kwenye mashine inayohusiana na kipengele cha kuperuzi baada ya kufunga, lakini hakuna mbinu za kuficha shughuli zako au alama zako za kidigitali mtandaoni. Hii humaanisha kuwa mtazamaji anaweza kukusanya uperuzi wako kwa urahisi kwenye browser yeyote.

Tor Bowser hutoa sifa zote za tab za faragha huku zikificha chanzo cha IP, mazoea ya kuperuzi na taarifa kuhusu kifaa ambacho kinaweza kutumika kama alama shughuli kwenye tovuti, kuruhusu uperuzi binafsi wa kweli ambayo imesimbwa .

Kwa taarifa zaidi juu ya vizuizi vya muundo wa Incognito na tab binafsi, tazama makala ya Mozilla kwenye Hadithi za kawaida kuhusu kuperuzi kwa faragha.

Kuna mbinu za mpangilio wa Tor Browser kama browser yako, lakini njia zote zinaweza zisifanye kazi kila mara au kwa kila mfumo wa uendeshaji. Kivinjari cha Tor hufanya kazi kwa bidii ili kujitenga na mfumo wako wote, na hatua za kuifanya kuwa kivinjari chaguo-msingi si za kutegemewa. Hii humaanisha muda mwingine tovuti ingepakia Kivinjari cha Tor, na muda mwingine itapakia katika kivinjari nyingine. Aina hii ya tabia inaweza kuwa hatari na kuvunja kutojulikana.

Tunapendekeza kutumia Tor sio kwenye kivinjari chochote ila tumia kwenye Tor Browser. Kutumia Tor kwenye kivinjari kingine inaweza kukuacha katika hatari bila ulinzi wa faragha wa Tor Browser.

Unaweza kutumia bowser nyingine huku ukitumia pia Tor Brower. Japokuwa, unatakiwa kujua mahitaji ya faragha ya Tor Browser haziwezi kuwepo katika browser nyngine. Kuwa makini unaporudi tena na kutoka nje kati ya Tor na browser yennye usalama mdogo, kwa sababu unaweza kwa bahati mabaya ukatumia browser nyingine kwa kitu fulani ulichatarajia kufanya ukitumia Tor.

Kama unatumia Tor Browser na kivinjari kingine kwa wakati mmoja, haita athili utendaji wa Tor au tabia ya faragha.

Hatahivyo, jua kwamba unapotumia Tor na kivinjari kingine kwa wakati mmoja, shughuli zako za Tor zinaweza kuingiliana na shughuli zisizo za Tor (halisi) IP kutoka katika kivinjari kingine, kwa kusogeza mausi yako toka katika kivinjari kimoja kwenda kingine.

Au unaweza kusahau kwa bahati mbaya ukatumia kivinjari kisicho na faragha kufanya jambo fulani ambacho umekusudia kufanya katika Tor Browser badala yake.

Historia ya uperuzi wa Tor Browser pekee itakwenda kwenye mtandao wa Tor. Applikesheni nyingine yeyote kwenye mfumo wako (ikiwemo browser nyingine) haitakuwa na mawasiliano katika mtandao wa To, na haitakuwa na ulinzi. Unatakiwa kusanidiwa tofauti kutumia Tor. Kama unahitaji kuwa na uhakika kuwa trafiki yote itakwenda kwenye mtandao wa Tor, tazama mfumo wa uendeshaji wa moja kwa moja wa Tails ambao unaweza kuanza kwenye kompyuta yeyote kutoka kwenye USB au DVD.

Hatupendekezi kutumia mifano mingi ya Tor browser, na kwa kufanya hivyo inaweza isifanye kazi kama ilivyotarajiwa katika platiform nyingi.

Tor Browser imetengenezwa kutumia Firefox, hivyo dosari kuhusu Firefox zinaweza kutokea. Tafadhali hakikisha hakuna mfano mwingine wa Tor Browser ulisha utumia, na utakua umejitoa katika eneo la Tor browser kuwa mtaumiaji wako ana ruhusa sahihi kwa ajili hiyo. Kama unatumia anti-vurus, tafadhali angalia Antivirus yangu/ ulinzi wa malware imenizuia kuipata Tor Browser , ni kawaida kwa programu za anti-virus/anti-malware kusababisha aina hii ya tatizo.

Tor Browser ni toleo lililo boreshwa la Firefox hususani imeundwa kwa matumizi na Tor. Kazi kubwa zimefanyika kuifanya Kivinajri chaTor, ikijumuisha utumiaji wa patch za ziada kuimarisha faragha na ulinzi. Kiufundi inawezekana kutumia Tor pamoja na vivinjari vingine, unaweza ukajiweka katika uwezekano wa kushambuliwa au kuvuja kwa taarifa, hivyo tunawakatisha tamaa kwa hilo. Jifunze zaidi kuhsu muundo wa Tor Browser.

Bookmarks in Tor Browser for Desktop can be exported, imported, backed up, restored as well as imported from another browser. The instructions are similar on Windows, macOS and Linux. Ili kuweza kusimamia vialamisho vyako kwenye Tor Browser, nenda kwa:

 • Menyu iliojificha>>alamisho>>simamia alamisho (chini ya menyu)
 • From the toolbar on the Library window, click on the option to 'Import and Backup'.

Makadirio sahihi ya Tor Browser na bookmarks

 • hamisha vilalamisho kwenye HTML
 • "- -- Katika dirisha la Faili ya Kutoa Vialamisho inayofunguliwa, chagua eneo la kuhifadhi faili, ambayo kwa chaguo-msingi inaitwa bookmarks.html. kompyuta ya mezani kawaida ni mahali pazuri, lakini mahali popote rahisi kukumbuka litafanya kazi.
 • Bonyeza kitufe cha Hifadhi. window ya kuweka Faili ya Alamisho litafungwa.
 • Funga maktaba ya window.

Vialamisho vyako kwa sasa vimefanikiwa kutoka Tor Browser. Faili la HTML la alamisho ulilohifadhi limekamilika sasa na linaweza kuagizwa kwenye kivinjari kingine cha wavuti.

kama unahitaji kuweka bookmark

 • ingiza alamisho kwa HTML
 • Ndani ya window ya kuingiza vialamisho linalofunguka, nenda kwenye faili ya HTML ya vialamisho unavyoingiza na uichague faili.
 • -Bonyeza kitufe cha Kufungua. Dirisha la Uingizaji wa Faili ya Alamisho litafungwa.
 • Funga maktaba ya window.

vialamisho vilivyochaguliwa kwenye faili la HTML itaongezwa kwenye Tor Browser yako kuhusiana na Bookmarks menu directory.

kama utahitaji kurudisha upya

 • Chagua Backup
 • window mpya itafunguka na unatakiwa kuchagua eneo kuhifadhi faili. liwe na .jsonextension.

kama unahitaji kuhifadhi tena

 • Chagua Rudisha na kisha chagua faili ya alamisho unayotaka kurejesha.
 • Bonyeza sawa kwenye kisanduku cha pop-up kinachoonekana na haraka, umeweza kurejesha alamisho lako la kurasa ulilolihifadhi.

Import bookmarks from another browser

Vialamisho vinaeza kusafirishwa kutoka firefox na Tor Browser. kuna njia mbili za kuingiza na kutoa vialamisho kwenye firefox: HTMLfile au faili la JSON. After exporting the data from the browser, follow the above steps to import the bookmark file into your Tor Browser.

Tahadhari: Kwa sasa, kwenye Tor Browser kwa Android, hakuna njia nzuri ya kusafirisha na kuingiza alamisho. Kosa #31617

Unapokuwa na Tor Browser wazi unaweza kuperuzi katika hamburger menu ("≡"), kisha bofya katika "Settings", na mwisho katika "Connection" upande wa pembeni. Chini katika kurasa, pembeni ya maandishi ya "View the Tor logs", bofya kitufe cha "View Logs...". Unatakiwa kuona chaguo la kunakili historia yako katika kurasa yako, amabayo utakuwa na uwezo wa kunakilisha katika ukurasa wa kuandikia au kutuma barua pepe kwa mtumiaji.

Njia mbadala, katika GNU/Linux, kuona tatizo hapohapo katika kifaa, peruzi katika saraka ya Tor Browserna ianzishe kutumia Tor Browser kutoka katika sehemu ya amri:

./start-tor-browser.desktop --verbose

au kutunza kumbukumbu katika faili (default: tor-browser.log)

./start-tor-browser.desktop --log [file]

Katika mfumo wake wa asili Tor Browser inaanza na kurasa ya maudhui yenye kiwango cha makadirio ya 200px x 100px ili kuzuia fingerprinting ya vipimo vya skrini. Mkakati unaotumika hapa ni kufanya watumiaji wote katika namna ambayo itakuwa ngumu kuwatoa nje. Hii hufanya kazi mpaka pale watumiaji watakapoanza kubadili ukubwa wa windo zao (mfano kwa kuzipinguza au kwenda katika muonekano wa skrini nzima). Tor Browser kuwa na ulinzi wa fingerprinting kwa matukio hayo pia, ambayo huitwa Letterboxing, mbinu iliyotengenezwa na Mozilla napresented in 2019. Inafanya kazi kwa kuongeza pambizo nyeupe katika kurasa ya kivinjari sababu kurasa inakuwa karibu sana katika ukubwa unaotakiwa wakati watumiaji wanakuwa katika ukubwa wa skrini zilizofungiwa ambazo zinazuia kuwatoa nje kwa msaada wa vipimo.

Kwa maneno rahisi, mbinu hii huweka watumiaji wengi wa aina fulani ya ukubwa wa skrini na hii hufanya kuwa na ugumu kwa mtumiaji mmoja kwa kuzingatia ukubwa wa skrini, sababu watumiaji wengimwatakuwa na skrini yenye ukubwa sawa.

letterboxing

Tor Browser inaweza kwa uhakika kuwasaidia watu kufika tovuti yako katika sehemu ambazo zimezuiliwa. Mara nyingi, Pakua kwa urahisi Tor Browser na uitumie kutafuta tovuti zilizozuiliwa ili kuruhusu kufikiwa. Katika maeneo yenye udhibiti mkali tuna machaguo kadhaa ya kukwepa udhibiti huo, ikiwemo pluggable transports.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali angalia Tor Browser User Manual section on censorship circumvention.

kunawakati tovuti itafunga watumiaji wa Tor kwasababu haziwez kuonesha tofauti kati ya usawa wa mtumiaji wa Tor na trafic ya kiautomatiki. Kwa mafanikio mazuri ni kupata ukurasa kwa watumiaji kuifungua Tor watumiaji watapata kuwasiliana na wasimamizi wa tovuti moja kwa moja. Kitu kama hiki inaweza kuwa ni ujanja:

"Habari!" nimejaribu kuifikia tovuti yako xyz.com huku nikitumia Tor Browser na nimegundua kwamba hujawaruhusu watumiaji wa Tor kuifikia tovuti yako. Nakuhimiza kuzingatia maamuzi haya: Tor hutumika na watu duniani kote kulinda faragha zao na kupinga udhibiti. Kwa kudhibiti watumiaji wa Tor, ni kama umewadhibiti watu katika nchi zao ambao wanataka kutumia mtandao wa bure, waandishi wa habari, watafiti ambao wanataka kujilinda wenyewe dhidi ya ugundunduzi, watoa taarifa, wanaharakati na watu wakawaida ambao wanataka kujiondoa kwenye wadukuzi. Tafadhali chukua msimamo mkali kwa kuzingatia faragha za kidigitali na uhuru wa mtandao na ruhusu watumiaji wa Tor kupata xyz.com. Ahsante"

Kwa kesi za bank, na tovuti nyingine muhimu, ni kawaida kuona udhibiti wa msingi wa jiografia (kama bank imejua umeweza kupata huduma zao kutoka nchi moja, na ghafla umejiunganisha na exit relay kwenye upande mwingine wa dunia, akaunti yako inaweza kudhibitiwa au kuondolewa).

Kama umeshindwa kujuinganisha na onion services, tafadhali tazama siwezi kuipata X.onion!.

Tor Browser inafanya muunganiko wako ujitokeze japo hutoka kwenye sehemu tofauti za dunia. Baadhi ya tovuti, kama vile bank au watoa huduma za email, wanaweza kutasfiri kuwa alama hii ni akaunti yako imeondolewa na kukufungia.

Njia pekee ya kutatua hili ni kufuata mapendekezo ya utaratibu wa tovuti ili kurejesha akunti au kuwasiliana na waeneshaji na uwaelezee hali hiyo.

Unaweza kuzuia hali hii kama mtoa huduma wako ametoa uthibitishaji wa awamu ya pili, ambayo ni ulinzi bora kuliko zifa za msingi za IP. Mtafute mtoa huduma wako na wauulize kama wanatoa 2A.

Muda mwingine tovuti nzito za JavaScript zinaweza kuwa na matatizo ya ufanyaji kazi katika Tor Browser. Namna ya kurekebisha kwa urahisi ni kubonyeza katika alama ya ulinzi (ngao ndogo za kijivu upande wa kulia juu ya kioo), kisha bonyeza "Badili..." Pangilia ulinzi wako kuwa "imara".

Ulinzi mwingi wa antivirus au programu hasidi huruhusu mtumiaji "kuorodhesha" michakato fulani ambayo ingezuiliwa. Tafadhali fungua programu yako ya kingavirusi au programu hasidi na utafute katika mipangilio ya "allowlist" au kitu kama hicho. Kufuatia, jumuisha michakato ifuatayo:

 • Kwa window
  • firefox.exe
  • tor.exe
  • lyrebird.exe (kama unatumia daraja)
  • snowflake-client.exe
 • Kwa macOS
  • TorBrowser
  • tor.real
  • lyrebird (kama unatumia daraja)
  • snowflake-watumiaji

Hatimae,anza tena Tor Browser. Hii inapashwa kurekebisha masuala uliyokumbana nayo. tafadhari kumbuka kwamba wateja wa antivirus, kama Kaspersky, pia anatakiwa afungiwe Tor katika nafasi ya firewall.

Baadhi ya programu ya antivirus zitatoa onyo la programu hasidi na/au udhaifu wakati kivinjari cha Tor kinapoanza. Kama umepakua Tor Browser kutokaour main website or used GetTor, and verified it, haya ni majibu yasiyo sahihi na huitaji kuwa na wasiwasi. Baadhi ya programu za antivirus huchukulia kwamba faili ambazo hazijatazamwa na watumiaji wengi ni za kushukiwa. Ili kuhakikisha kuwa programu ya Tor unayopakua ni ile tuliyounda na haijasasishwa na mshambuliaji yeyote, unaweza kuhakiki saini ya Tor Browser.. unaweza pia kutaka kuruhusu mfumo wowote]kuzuia antiviruses kufunga ufikiaji wa Tor Browser.

Ikiwa muunganisho wako wa intaneti unaweza kuwa unazuia mtandao wa Tor, unaweza kujaribu kutumia viungo. Baadhi ya viungo vimejengwa katika Kivinjari cha Tor na vinahitaji hatua chache kuwezesha. Kutumia pluggable transport, bofya "Configure Connection" unapoanza kutumia Tor Browser kwa mara ya kwanza. Chini ya sehemu ya "Bridges", onyesha chaguo la "Choose from one of Tor Browser's built-in bridges" na bofya katika chaguo la "Select a Built-In Bridge". Kutoka katika mpangilio, chagua chochote pluggable transport utakachopenda kukitumia.

Pale unapokuwa umechagua pluggable transport, pandisha juu na bofya "Connect" kuhifadhi mpangilio.

Au, kama unatumia Tor Browser, Bonyeza "Settings" katika menu iliyofichwa (≡) na halafu "Connection" katika ubao wa pembeni. Chini ya sehemu ya "Bridges", onyesha chaguo la "Choose from one of Tor Browser's built-in bridges" na bofya katika chaguo la "Select a Built-In Bridge". Chagua pluggable transport wowote ungependa kutumia kutoka katika muongozo. Mpangilio wako utahifadhiwa otomatiki pale tu utakapofunga kurasa.

Ikiwa unahitaji bridges nyingine, unaweza kupata katika Bridges website yetu. Kwa taarifa zaidi kuhusu bridges, angalia Tor Browser manual.

Moja ya masuala ya kawaida ambayo husababisha makosa ya unganisho kwenye Tor Broswer ni mfumo wa saa usio sahihi. Tafadhari hakikisha mfumo wa saa na majira zimewekwa kwa usahihi. Kama hii haitatui tatizo, angalia Troubleshooting page on the Tor Browser manual.

Wakati mwingine, baada ya kutumia Gmail kwenye Tor, Google inawasilisha tarifa kwamba huenda akaunti yako imeingiliwa. Sehemu ya taarifa huorodhesha mfululizo wa anwani za IP na maeneo ulimwenguni sasa hutumika kupata akaunti yako.

Kwa ujumla, hii ni kengele isiyosahihi: Google iliona kundi lililoingia katika sehemu tofauti, kama matokeo ya kuendesha huduma kupitia Tor, na kuamua ilikua wazo zuri la kuhakikisha akaunti itafikiwa na mmiliki wake halali.

Japokuwa hii inaweza kuwa ni kutokana na utumiaji wa huduma kupitia Tor, hii haimaanishi unaweza kudharau angalizo. Inawezekana ni uwongo chanya, lakini haiwezi kwa kuwa inawezekana kuna mtu ameteka cookie zako za Google.

Utekaji wa cookie unawezekana kwa njia ya kuipata compyuta yako au kuangalia upekuzi wa mtandao wako. Kwa nadharia,ufikiaji wa kawaida pekee unaweza kuelewana na mfumo wako kwasababu Gmail na huduma za kipekee zinzweza kukutumia cookie juu ya muunganiko wa SSL. Kwa vitendo, alas, ni way more complex than that.

Na kama kuna mtu ameiba cookie zako za Google, wataishia kuingia kwenye sehemu zisizo za kawaida (pia wanaweza wasiingie). Kwa ufupi ni kwamba ukiwa unatumia Tor Browser, mbinu hii ya ulinzi ambayo Google hutumia haikufai, kwa sababu imejaa chanya za uwongo. Unatakiwa utumie mbinu nyingine, kama vile kuona kama kuna kitu chochote kinaonekana cha ajabu katika akaunti, au kinaonekana katika hifadhi ya waliongia hivi karibuni na unashangaa kama umeingia katika muda huo.

Hivi karibuni, watumiaji wa Gmail wanaweza kuwasha hatua ya 2 ya uthibitishho katika akaunti zao kuongeza safu ya ziada ya ulinzi.

Hili linajulikana na huonysha tatizo; haimaanishi kwamba Google huiona Tor kama ni spyware.

Utakapo iona Tor yako, unatuma maswali kupita exit relay ambazo zimesambazwa na maelefu ya watumiaji wengine. Watumiaji wa Tor wanaona ujumbe huu pale watumiaji wengi wa Tor wanapouliza Google kwa muda mfupi. Google hukatiza kiwango cha juu cha traffic katika anwani ya IP moja (exit relay uliyoichagua) kama mtu anayejaribu kufuatiza tovuti, hizo inapunguza traffick kutoka kwenye anwani ya IP kwa muda mfupi.

Unaweza kujaribu Circuit mpya kwa tovuti hii kuzipata tovuti kutoka kwenye anwani za IP tofauti.

Maelezo mbadala ni kwamba Google hujaribu kugundua aina fulani za spyware au virus ambazo hutuma maswali tofauti katika ukurasa wa kutafuta wa Google. Inakumbuka anwani za IP kutoka kwenye maswali yote yaliyopokelewa (hawajagundua kuwa ni exit relay za Tor), na wanajaribu kutoa angalizo kwa mawasiliano yoyote yanayotoka kwenye anwani za IP ambazo maswali ya hivi karibuni huonyesha tatizo.

Kwa uwezo wetu, Google haifanyi kitu chochote kwa kukusudia hususani kuzuia au kudhibiti matumizi ya Tor. Ujumbe wa dosari kuhusu mashine iliyoathirika itafutika baada ya muda mfupi.

Kwa bahati mbaya, baadhi ya tovuti hutoa Captcha kwa watumiaji wa Tor, na hatuwezi kuondoa Captcha hizo kwenye tovuti. Kitu bora cha kufanya katika changamoto hizi ni kuwasiliana na wamiliki wa tovuti, na uwataarifu kwamba Captcha zao zimezuia watumiaji kama vile wewe kutumia huduma zao.

Google hutumia "eneo la kijographia" kutambua upo wapi duniani, hivyo inaweza kukupa uzoefu binafsi. Hii huusisha utumiaji wa lugha inadhani unapendelea, pia inahusisha kukupa matokeo tofauti ya maswali yako.

Kama unataka kuonga Google kwa lugha ya kiingereza unweza kugusa link ambayo inatoa lugha hiyo. Lakini tunazingatia sifa za Tor, na sio tatizo--- Mtandao sio tambarare, na kiuhalisia huonekana tofauti inategemea na wapi ulipo. Sifa hizi hukumbusha watu kuhusu hili.

Zingatia URL za Google search huchukua jina/ thamani ya jozi za hoja na moja ya majina hayo ni "hl". Kama unatuma "hl" kwenda "en" ndipo Google watakurudishia matokea kwa lugha ya kiingereza bila kujali ni Google seva ipi umetuma. Link iliyobadilika inaweza kuonekana kama hivi:

https://encrypted.google.com/search?q=online%20anonymity&hl=en

Mbinu nyingine ni kurahisisha msimbo wa nchi yako ili kupata Google. Hii inaweza kuwa google.be, google.de, google.us na nyinginezo.

Unapotumia Tor Browser, hakuna anaye weza kuona tovuti ulizotemebelea. Japokua, mtoa huduma wako au muendesha matandao anaweza kuona kuwa umejuinganisha na mtandao wa Tor, japokuwa hahawezi kujua nini unafanya unapokuwa huko.

Tor Browser inazuia watu kujua tovuti unayotembelea. Baadhi ya vitu, kama vile watoa huduma wa mtandao wako (ISP), wanaweza kujua kuwa unatumia Tor, lakini hawawezi kujua unachokifanya na unapotembelea.

DuckDuckGo ni chaguo msingi kutafuta injini kwenye Tor Browser. DuckDuckGo haifuatilii watumiaji wake wala haiifadhi data yoyote kuhusiana na kuperuzi kwa watumiaji wake. Soma zaidi kuhusu DuckDuckGo privacy policy.

Katika toleo la Tor Browser la 6.0.6, tulihamisha kwenda DuckDuckGo kama injini ya msingi ya utafutaji. Kwa muda sasa, Tenganisha, ilikua inatumika kwenye Tor Browser, ilikua haiwezi kupata matokeo ya Google search. Tangu Tenganisha ni zaidi ya utafutaji wa injini ya Meta, ambayo inaruhusu watumiaji kuchagua kati ya watoa huduma za utafutaji tofauti, itarudi nyuma kuleta matokeo ya utafutaji wa Bing, ambayo hayakukubalika ubora wake. DuckDuckGo haingii, hukusanya au sambaza taarifa binafsi za mtumiaji au historia yao ya walivyotafuta, na hivyo ni nafasi bora kulinda faragha yako. Injini nyingine nyingi za kuuliza vitu huifadhi ulivyovitafuta na taarifa nyingine kama vile muda uliotafuta, anwani yako ya IP na taarifa za akaunti yako kama uliingia.

Tafadhali angalia DuckDuckGo support portal. Ikiwa una amini hili ni tatizo la Tor Browser, Tafadhali toa taarifa kwenye issue tracker.

Tor Browser ina njia mbili za kubadili relay circuit yako — "New Identity" na"New Tor Circuit kwa ajili ya tovuti". Chaguzi zote zimeelekezwa kwenye hamburger menu ("≡"). Pia unaweza kupatachaguo la New Circuit ndani ya menyu ya taarifa za tovuti sehemu ya kuandikiaURL, na chagua la the New Identity kwa kubofya nembo ya small sparky broom upande wa juu kulika katika skrini yako.

New Identity

Chaguo hili linafaa kama unataka kuzuia shughuli zako za kuperuzi za baadae kuunganishwa na ulichokuwa unafanya kabla.

Kuchagua itafunga tab zako zote na window, futa habari zote za kibinafsi kama vile cookies na historia za browsing,na utumie mzunguko wa Tor kwenye munganiko wako wowote.

Tor Browser itakutahadharisha kuwa shughuli zote na upakuaji utasitishwa, kwa hiyo zingatia hili kabla ya kubofya "New Identity".

Tor Browser Menu

mpya kwenye ukurasa huuTor Circuit

Chagua hili linafaa kama exit relay unayotumia haiwezi kuunganishwa katika tovuti unayoihitaji, au haichakati ipasavyo. Kuichagua itasababisha tab inayotumika kwa sasa au window kupakiwa upya Tor circuit.

Kurasa zingine zilizowazi na window kutoka kwenye tovuti moja itatumia circuit mpya vilevile tu mara zitakapopakiwa upya.

Chaguo hilihalifuti taarifa zozote za faragha au kutenganisha shughuli zako, walahaiharibu uhusiano wako wa sasa kwenye tovuti.

Mpya kwenye ukurasa huu Circuit

Utumiaji wa Tor Browser haikufanyi uigize ni relay katika mtandao. Hii inamaanisha kwamba kompyuta yako haitatumika kuchunguza wengine. Kama unataka kuwa relay, tafadhali tazama muongozo wa Tor relay zetu.

Hiyo ni tabia ya kawaida ya Tor. Relay ya kwanza katika circuit yako inaitwa "guard ya kuingia" au "guard". Ni relay ya haraka na imaraambayo inabaki kuwa ya kwanza katika circuit yako kwa miezi 2-3 ili kulinda faragha inayojulikana kuvamiwa. Mabadiliko mengine ya circuit yako kwa kila tovuti mpya unayotembelea, na zote kwa pamoja relays hizi hutoa ulinzi kwa Tor. Kwa taarifa zaidi ya namna guard relays zinafanya kazi, angalia hii blog post na paper katika guards ya kuingia.

Kwenye Tor Browser, kila kikoa kipya inapata circuit yake. Muundo na utekelezaji wa Tor Browser imeelezea kuhusu kufikiria juu ya muundo huu.

Kurekebisha njia ambayo Tor hujenga nyaya zake imekata tamaa. Unapata ulinzi bora ambao Tor inaweza kukupatia unapoacha uchaguzi wa usafirishaji katika Tor; kutumia sana/node ya kutoka inaweza kukubaliana na kutojulikana. Kama matokeo unayoyataka ni kupata vitu vilivyopo zilizopo katika nchi moja tu, unaweza kuhitaji kuzingatia kutumia VPN badala ya kutumia Tor. Tafadhali zingatia VPNs haina tabia za faragha kama za Tor, lakini zitatatua baadhi ya vizingiti vya eneo.

TAHADHARI: USIFUATE maelekezo yasiyo katika mpangilio ili kuhariri torrc yako! Kufanya hivyo kunaweza kuruhusu mshambuliaji kuondoa ulinzi wako na kutojulikana kwako kupitia programu hatari za malicious kwenye torrc yako.

Tor hutumia faili la maandishi linaloitwa torrc ambalo lina maelekezo ya kusanidi namna Tor inatakiwa kufanya kazi. Usanidi wa asili unatakiwa kufanya kazi vema kwa watumiaji wengi wa Tor(Ndipo tahadhali ya hapo juu.)

Ili kupata Tor Browser torrc yako, fuata maelekezo katika kifaa chako hapo chini.

Kwenye Window au Linux:

 • Torrc ipo kwenye ipo kwenye muongozo wa data wa Tor Browser kwenye Browser/TorBrowser/Data/Tor ndani ya Tor muongozo wa Tor Browser yako.

Kwenye macOS:

 • Torrc ipo kwenye muongozo wa data ya Tor Browser kwenye ~/Library/Application Support/TorBrowser-Data/Tor.
 • Zingatiathe Folda la maktaba limefichwa katika toleo jipya la macOS. Kulitafuta hili foldar, chagua "Go to Folder..." katika menyu ya "Go".
 • Kisha andika ~/Library/Application Support/ katika windo kisha bofya Go.

Funga Tor Browser kabla ya kuhariri torrc yako, vinginevyo Tor Browser inaweza kuondoa uboreshaji wako. Chaguo zingine hazitakua na madhar kama Tor Browser huzipatilisha kwa amri ya safu za chaguzi wakati Tor inaanza.

Pitia kwenye faili la mifano yatorrc kwa vidokezo juu ya usanidi wa kawaida. Kwa machaguo mengine ya usanidi unaweza kutumia , tazama ukurasa wa muongozo wa Tor. Kumbuka, mistari yote imeanza na # kwenye torrc inachukuliwa kama maoni na hakuna madhara yeyote kwenye usanidi Tor.

Inakatisha tamaa kuongeza matangazo kwenye Tor Browser, kwa sababu inaweza kuondoa faragha na ulinzi wako.

Kuongeza matangazo yanaweza kuathiri Tor Browser kwa njia zisizowezekana na inaweza kufanya kumbukumbu zako za Tor Browser ziwe za kipekee. Kama nakala yako ya Tor Browser ina kumbukumbu za uperuzi za kipekee, shughuli zako za uperuzi unaweza kudukuliwa japokuwa unatumia Tor Browser.

Kila mpangilio wa kivinjari na vipengele hutengeneza kitu kinachoitwa "alama ya kidole ya kivinjari". Browser nyingi bila kukusudia hutengeneza kumbukumbu za kipekee kwa kila mtumiaji ambazo zinaweza kudukuliwa kwenye mtandao. Tor Browser imejikita kuwa na kumbukumbu karibu sawa na watumiaji. Hii humaanisha kwamba kila mtumiaji wa Kivinjari cha Tor huonekana kama mtumiaji mwingine wa kivinjari cha Tor hufanya iwe ngumu kumdukua mtumiaji yeyote.

Pia kuna nafasi nzuri ya tangazo jipya inaweza kuongeza ushambuliaji wa Tor Browser. Hii inaweza kuruhusu taarifa muhimu kujuva au kuruhusu mshambuliaji kuathiri Tor Browser. Matangazo yenyewe yanaweza kuwa ni hatarishi yametengenezwa kukupeleleza.

Tor Browser inakuja na tangazo moja-NoScript- na kuongeza kitu kingine chochote kinaweza kuondoa kutojulikana kwako.

Unataka kujifunza zaidi kuhusu kumbukumbu za kuperuzi? Hii hapa ni makala katika blog ya Tor kuhusu hilo.

Flash haijawezeshwa kufanya kazi kwenye Tor Browser, na tunapendekeza usiiwezeshe. Hatudhani kuwa Flash ni salama kutumia katika browser yeyote- Ni programu ambayo haina ulinzi ambayo ni rahisi kuondoa faragha yako au kukuweka katika program hatarishi. Kwa bahati nzuri, tovuti nyingi, vifaa na vivinjari vingine hupotea kwa utumiaji wa Flash.

Kama unatumia Tor Browser, unaweza kuweka anuani yako ya proxy,port, na uthibitisho wa taarifa kwenye Connection Settings.

Ikiwa unatumia njia nyingine ya Tor, unaweza kuweka taarifa ya proxy kwenye faili lako la torrc. Angalia kwenye HTTPSProxy chaguo la usaidizi kwenye ukurasa wa muongozo. ikiwa umeomba udhibitisho wako, angali chaguo la HTTPSProxyAuthenticator . mfano na udhibitishaji:

 HTTPSProxy 10.0.0.1:8080
 HTTPSProxyAuthenticator myusername:mypass

Tunatumia uthibitishaji wa msingi pekee kwa sasa, lakini ikiwa unataka udhibitisho wa NTL, unaweza kutafuta kumbukumbu hii ya chapishoimetumika.

Kwa kutumia SOCKS proxy, see the Socks4Proxy, Socks5Proxy, inapelekea uchaguzi wa torrc kwenye muongozo wa ukurasa. Tumia SOCKS 5proxy uthibitisho unaweza kuonekana kama hivi:

 Socks5Proxy 10.0.0.1:1080
 Socks5ProxyUsername myuser
 Socks5ProxyPassword mypass

Ikiwa prox yako inakuruhusu tu kuungana na port fulani, angalia kingilio kwenye Firewalledwatumiaji kwa jinsi port ipi ya Tor itajaribu kuifikia.

Tafadhali angalia HTTPS Everywhere FAQ. Ikiwa unaamini hii ni Tor Browser kwa tatzo la Android, tafadhali toa taarifa kwenyeissue tracker.

Tangu Tor Browser 11.5,Hali pekee ya -HTTPS inawezeshwa na asili yake kwenye Kompyuta, na HTTPS Everywhere haijiunganishi tena na Tor Browser.

Tunasanidi NoScript kuruhusu JavaScript kwa asili yake katika Tor Browser kwa sababu tovuti nyingi hazitafanya kazi na JavaScript zilizoshindwa kufanya kazi. Watumiaji wengi, watakata tamaa na Tor kama hatutawezesha JavaScript kwa asili yake kwa sababu itasababisha matatizo mengi kwao. Hatimaye, tunataka kufanya Tor Browser iwe salama kadri iwezekanavyo huku ukiendelea kutumika na watu wengi, kwa sasa, inamaanisha kuondoa JavaScript inawezeshwa kwa asili yake.

Kwa watumiaji wanotaka kuwa na JavaScript isiyofanyekazi katika tovuti zote za HTTP kwa asili yake, tunapendekeza badilisha "kiwango cha ulinzi" katika Tor Browser yako. Hii inaweza kufanywa kwa kusafirisha alama ya ulinzi (ngao ndogo ya kijivu kwenye sehemu ya juu ya kulia ya kioo), kisha bonyeza "Change...". "Kiwango cha kawaida" uruhusu JavaScript, kiwango "salama" uzuia JavaScript kwenye tovuti za HTTP na kiwango salama zaidi huzuia JavaScript zote pamoja.

Ndio. Tor inaweza kusanidiwa kama mtumiaji au relay katika mashine nyingine, na kuruhusu mashine nyingine kuwezesha kujiunga kwa kutojulikana. Hii ni muhimu zaidi katika mazingira ambayo compyuta nyingi zinataka njia za kutojulikana uliwenguni kote. Hatahivyo, tambua kwanza kwa usanidi huu, yoyote katika mtandao wako binafsi (iliyopo kati kyako na mtumiaji wa Tor) inaweza kuona data zinazosafirishwa katika maandishi ya wazi. Kutojulikana kutaanza pale tu utakapofika katika Tor relay. Kutokana na hili, kama wewe ni muendeshaji wa kikoa chako na unajua kila kitu kilichozuiliwa, utakuwa sawa lakini usanidi huu hauwezi kufaa kwa mitandao mikubwa binafsi pale ambapo funguo za ulinzi ziko karibu.

Usanidi ni rahisi, kurekebisha faili lako la torrc SocksListenAddress kutokana na mifano ifuatayo:

SocksListenAddress 127.0.0.1
SocksListenAddress 192.168.x.x:9100
SocksListenAddress 0.0.0.0:9100

Unaweza kuweka anwani nyingi za listern, kama ni sehemu ya baadhi ya mitandao.

SocksListenAddress 192.168.x.x:9100 #eth0
SocksListenAddress 10.x.x.x:9100 #eth1

Baada ya hii, watumiaji wako katika mitandao yao husika wata bainisha socks proxy na anwani na port uliyobainisha kuwa anwani ya SocksListern. Tafadhali zingatia machaguo ya kusanidi SocksPort hutoa kifaa pekee cha localhost (127.0.0.1). Unapotengeneza anwani yako ya SocksListern (es), unatakiwa kutoa poti na anwani kama ilivyoonyeshwa hapo juu. Kama unapenda kulazimisha data zote zinazotoka kwa kupitia Tor relay kuu, badala ya seva pekee anza na proxy ya ziada, unaweza kupata programu inayofaa ya iptables (for *nix).

Kwa asili yake, mteja wako wa Tor anasikiliza tu applikesheni ambazo zimeunganishwa na mendeshaji wa ndani. Mawasiliano na kompyuta nyingine zimekataliwa. Kama unataka kutumia aplikesheni kwenye kompyuta nyingi kuliko mteja wa Tor, unaweza kuhariri torrc zako kuelezea anwani ya SocksListern 0.0.0.0 pia anzisha upya Tor. Kama unataka kupata iliyo bora zaidi, unaweza kusanidi mteja wako wa Tor ulinzi imara kujenga anwani yako ya IP ya ndani na sio anwani yako ya nje ya IP.

Tafadhali angalia NoScript FAQ. Ikiwa unaamini hili ni tatizo la Tor Browser, tafadhali toa taarifa kwenye bug tracker.

It is often important to know what version of Tor Browser you are using, to help you troubleshoot a problem or just to know if Tor Browser is up to date. This is important information to share when raising a support ticket.

Tor Browser Desktop

 • When you have Tor Browser running, click on "Settings" in the hamburger menu (≡).
 • Scroll down to the "Tor Browser Updates" section where the version number is listed.

Tor Browser ya Android

From the app

 • When you have Tor Browser for Android running, tap on 'Settings'.
 • Scroll to the bottom of the page.
 • Tap on 'About Tor Browser'.
 • The version number should be listed on this page.

From Android menu

 • Navigate to Android's Settings.
 • Tap on 'Apps' to open the list of apps installed on your device.
 • Find 'Tor Browser' from the list of apps.
 • Tap on 'Tor Browser'.
 • Scroll down to the very bottom of the page where the version number will be listed.