Ndio. Tor inaweza kusanidiwa kama mtumiaji au relay katika mashine nyingine, na kuruhusu mashine nyingine kuwezesha kujiunga kwa kutojulikana. Hii ni muhimu zaidi katika mazingira ambayo compyuta nyingi zinataka njia za kutojulikana uliwenguni kote. Hatahivyo, tambua kwanza kwa usanidi huu, yoyote katika mtandao wako binafsi (iliyopo kati kyako na mtumiaji wa Tor) inaweza kuona data zinazosafirishwa katika maandishi ya wazi. Kutojulikana kutaanza pale tu utakapofika katika Tor relay. Kutokana na hili, kama wewe ni muendeshaji wa kikoa chako na unajua kila kitu kilichozuiliwa, utakuwa sawa lakini usanidi huu hauwezi kufaa kwa mitandao mikubwa binafsi pale ambapo funguo za ulinzi ziko karibu.

Usanidi ni rahisi, kurekebisha faili lako la torrc SocksListenAddress kutokana na mifano ifuatayo:

SocksListenAddress 127.0.0.1
SocksListenAddress 192.168.x.x:9100
SocksListenAddress 0.0.0.0:9100

Unaweza kuweka anwani nyingi za listern, kama ni sehemu ya baadhi ya mitandao.

SocksListenAddress 192.168.x.x:9100 #eth0
SocksListenAddress 10.x.x.x:9100 #eth1

Baada ya hii, watumiaji wako katika mitandao yao husika wata bainisha socks proxy na anwani na port uliyobainisha kuwa anwani ya SocksListern. Tafadhali zingatia machaguo ya kusanidi SocksPort hutoa kifaa pekee cha localhost (127.0.0.1). Unapotengeneza anwani yako ya SocksListern (es), unatakiwa kutoa poti na anwani kama ilivyoonyeshwa hapo juu. Kama unapenda kulazimisha data zote zinazotoka kwa kupitia Tor relay kuu, badala ya seva pekee anza na proxy ya ziada, unaweza kupata programu inayofaa ya iptables (for *nix).