Maswali yanayoulizwa sana

Tor Browser inazuia watu kujua tovuti unayotembelea. Baadhi ya vitu, kama vile watoa huduma wa mtandao wako (ISP), wanaweza kujua kuwa unatumia Tor, lakini hawawezi kujua unachokifanya na unapotembelea.

Kwa ujumla ni haiwezekani kutokujulikana kabisa, hata kwa Tor. Ingawa kuna baadhi ya mambo unaweza kufanyia mazoezi ili kuboresha kutokujulikana kwako wakati unatumia Tor na ukiwa nje ya mtandao.

Tumia Tor Browser na programu muhsusi iliyosanidiwa na Tor

Tor haiwezi kulinda muingiliano yote ya mtandao wa intaneti wa kompyuta yako unapoendesha programu hiyo. Tor inalinda programu tu ambazo zimefanyiwa usanidi sahihi wa usafirishaji wa data kupitia Tor.

Kuvinjari tovuti:

Kusambaza faili:

Dhibiti maelezo unayotoa kupitia fomu za tovuti

Ikiwa utatembelea tovuti kwa kutumia Tor Browser, hawatafahamu wewe nani au sehemu yako sahihi ulipo. Japokuwa tovuti nyingi huuliza zaidi juu ya taarifa binafsi kuliko wanavyohitaji kupitia fomu za tovuti. Ikiwa utangia katika tovuti hiyo, bado hawataweza kujua sehemu uliyopo lakini watajua wewe ni nani. Zaidi ya hayo, utatoa: jina, barua pepe, anwani, namba ya simu, au taarifa zingine binafsi, hautakuwa tena mtu usiyejulikana katika tovuti hiyo. Njia nzuri ya kujilinda ni kuwa makini na kuchukua tahadhari kipindi unajaza fomu za tovuti.

Usitumie torrent na Tor

faili kwa njia ya Torrent zimeonekana kupuuza mipangilio ya proksi na kufanya mawasiliano moja kwa moja hata wanapoelekezwa kutumia Tor. Hata kama programu yako ya torrent imeunganishwa kupitia Tor pekee, unaweza kutana mara chache anwani yako halisi ya IP katika ombi la GET ya tracker, kwa sababu ndivyo torrent inafanya kazi. Sio wewe tu Ondoa utambulisho wa usafirishwa wa data ya torrent na mfuatao mwingine wa usafirishwaji wa data wa tovuti ya Tor njia hii, utapunguza kasi ya mtandao mzima wa Tor kwa kila mtumiaji.

Usiwezeshe au kusanikisha browser plugins

Tor Browser itazuia programu ya kivinjari kama vile Flash, RealPlayer, Quicktime na nyinginezo: zinaweza kuendeshwa kuonyesha anwani yako ya IP. Vile vile, hatupendekezi kusanikisha nyongeza ya addons au plugins kwenye Tor Browser, kwani hizi zinaweza kukwepa Tor au vinginevyo kudhuru kutokujulikana kwako na faragha.

Tumia toleo la HTTPS la tovuti

Njia ya Tor itahifadhi data yako kwa kutumia teknolojia ya kusimba, ndani na nje ya mtandao wa Tor, lakini usimbaji wa usafirishaji wa data yako kwenda kwenye tovuti ya mwisho unategemeana na tovuti husika. Ili kusaidia kuhakiki usimbaji wa tovuti, Tor Browser ikiwemo HTTPS-Only Mode kulazimisha kututumia HTTPS iliyosimbwa katika tovuti inayoiunga mkono. Walakini, unaweza kuendelea kuangalia anwani ya URL katika browser ambayo inawezesha tovuti kukupata taarifa nyeti ili kuzionesha padlock au onion icon katika sehemu ya kuandika anwani, ikiwemo https:// katika URL, na kuonesha jina sahihi linalotarajia na tovuti. Pia angalia michoro ya EFF inayoingiliana ikielezea jinsi Tor na HTTPS zinavyohusiana.

Usifungue nyaraka iliyopakuliwa kupitia Tor ukiwa mtandaoni

Tor Browser kitakuonya kabla ya kufungua moja kwa moja hati ambazo zinasimamiwa na programu za nje. USIPUUZE ONYO HILI. Unapaswa kuwa makini wakati unapopakua nyaraka kupitia Tor (hususani DOC na mafaili ya PDF, isipokuwa unapotumia PDF viewer iliyotengenezwa katika Tor Browser) nyaraka hizi zinaweza kukusanya vyanzo vya mtandao ambavyo vitapakuliwa nje ya Tor kwa kutumia programu tumizi inayozifungua. Hii itaonesha anwani yako ya IP isiyo ya Tor. Ikiwa lazima utashughulika mafaili yaliyopakuliwa kupitia Tor tunapendekeza sana ama kutumia kompyuta ambayo haijaunnganisha, au kutumia dangerzone kutengeneza mafaili ya PDF salama ambayo utaweza kuyafungua. Hata hivyo, bila ya kuwa na sababu ya msingi ni salama kuitumia BitTorrent na Tor kwa pamoja.

Tumia bridges na/au tafuta kampuni

Tor inajaribu kuzuia wadukuzi kujifunza ni tovuti zipi umejiunganisha nazo. Walakini, kwa chaguo la msingi, haimzuii mtu anaye kutazama katika usafirishwaji wa data za mtandao kwa kujifunza kwamb unatumia Tor. Ikiwa hii ni muhimu kwako, unaweza kupunguza hatari kwa kusaidi Tor kwa kutumia bridge badala ya kuuunganisha moja kwa moja katika mtandao wa Tor. Mwishoni njia nzuri ya ulinzi ni mbinu ya kijamii: kadri watumiaji wa Tor wavyoongezeka wanakuwa karibu na wewe na maslahi tofauti zaidi yako, hatari inakuwa ndogo ukiwa mmoja wao. Washawishi watu wengine watumie Tor, pia!

Kuwa nadhifu na jifunze zaidi. Elewa nini Tor inafanya na ambacho haikifanyi. Orodha hii ya mitego haijakamilika, na tunahitaji msaada wako kutambua na kuweka kumbukumbu wa mambo yote.

Tor Browser kwa sasa inapatikana kwenye Windows, Linux, macOS na Android.

Kwenye Android, Mradi wa Guardian pia hutoa programu ya Orbot kuelekeza programu zingine kwenye kifaa chako cha Android kupitia mtandao wa Tor.

Hakuna toleo rasmi la Kivinjari cha Tor kwa iOS bado, kama ilivyoelezwa katika chapisho hili la blogu. Pendekezo letu bora linalopatikana ni Kivinjari cha Onion.

Inakatisha tamaa kuongeza matangazo kwenye Tor Browser, kwa sababu inaweza kuondoa faragha na ulinzi wako.

Kuongeza matangazo yanaweza kuathiri Tor Browser kwa njia zisizowezekana na inaweza kufanya kumbukumbu zako za Tor Browser ziwe za kipekee. Kama nakala yako ya Tor Browser ina kumbukumbu za uperuzi za kipekee, shughuli zako za uperuzi unaweza kudukuliwa japokuwa unatumia Tor Browser.

Kila mpangilio wa kivinjari na vipengele hutengeneza kitu kinachoitwa "alama ya kidole ya kivinjari". Browser nyingi bila kukusudia hutengeneza kumbukumbu za kipekee kwa kila mtumiaji ambazo zinaweza kudukuliwa kwenye mtandao. Tor Browser imejikita kuwa na kumbukumbu karibu sawa na watumiaji. Hii humaanisha kwamba kila mtumiaji wa Kivinjari cha Tor huonekana kama mtumiaji mwingine wa kivinjari cha Tor hufanya iwe ngumu kumdukua mtumiaji yeyote.

Pia kuna nafasi nzuri ya tangazo jipya inaweza kuongeza ushambuliaji wa Tor Browser. Hii inaweza kuruhusu taarifa muhimu kujuva au kuruhusu mshambuliaji kuathiri Tor Browser. Matangazo yenyewe yanaweza kuwa ni hatarishi yametengenezwa kukupeleleza.

Tor Browser inakuja na tangazo moja-NoScript- na kuongeza kitu kingine chochote kinaweza kuondoa kutojulikana kwako.

Unataka kujifunza zaidi kuhusu kumbukumbu za kuperuzi? Hii hapa ni makala katika blog ya Tor kuhusu hilo.

Kwa ujumla, hatupendekezi kutumia VPN na Tor isipokuwa wewe ni mtumiaji mwenye ujuzi zaidi anajua jinsi ya kusanidi pande zote kwa njia ambayo haihatarishi faragha yako.

Unaweza kupata taarifa zaidi za Tor+VPN katika awani yetu wiki.

Tor Browser inaweza kwa uhakika kuwasaidia watu kufika tovuti yako katika sehemu ambazo zimezuiliwa. Mara nyingi, Pakua kwa urahisi Tor Browser na uitumie kutafuta tovuti zilizozuiliwa ili kuruhusu kufikiwa. Katika maeneo yenye udhibiti mkali tuna machaguo kadhaa ya kukwepa udhibiti huo, ikiwemo pluggable transports.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali angalia Tor Browser User Manual section on censorship circumvention.

Hakika, Tuna Orodha ya mashirika yanayotumia Tor relays ambayo yatafurahia kubadilisha michango yako kuwa kasi bora ya kutojulikana kwa mtandao wa Tor.

Mashirika haya hayapo sawa na The Tor Project, Inc, lakini tuna zingatia kuwa ni kitu kizuri. Zinaendeshwa na watu wazuri ambao ni sehemu ya jumuiya ya Tor.

Kumbuka kuwa kunaweza kuwa na kukubaliana kati ya kutojulikana na kiwango cha utendaji kazi. Kutokujulikana kwa mtandao wa Tor huja kwa sehemu kutoka kwa utofauti, hivyo ikiwa katika sehemu ya kutumia relay yako, utaboresha Kutokujulikan kwa Tor zaidi kwa kuchangia. Ingiwa katika wakati huo, uchumi wa kipimo cha kiwango cha data unamaanisha kuchanganya michango mingi midogo katika relay kadhaa kubwa kuna ufanisi mkubwa katika kuboresha utendaji wa mtandao. Kuboresha kutokujulina na kuboresha utendaji zote kwa pamoja huleta malengo yenye thamani, hata hivyo unaweza kusaidia pakubwa!