Kwa bahati mbaya, baadhi ya tovuti hutoa Captcha kwa watumiaji wa Tor, na hatuwezi kuondoa Captcha hizo kwenye tovuti. Kitu bora cha kufanya katika changamoto hizi ni kuwasiliana na wamiliki wa tovuti, na uwataarifu kwamba Captcha zao zimezuia watumiaji kama vile wewe kutumia huduma zao.