Ulinzi mwingi wa antivirus au programu hasidi huruhusu mtumiaji "kuorodhesha" michakato fulani ambayo ingezuiliwa. Tafadhali fungua programu yako ya kingavirusi au programu hasidi na utafute katika mipangilio ya "allowlist" au kitu kama hicho. Kufuatia, jumuisha michakato ifuatayo:

 • Kwa window
  • firefox.exe
  • tor.exe
  • lyrebird.exe (kama unatumia daraja)
  • snowflake-client.exe
 • Kwa macOS
  • TorBrowser
  • tor.real
  • lyrebird (kama unatumia daraja)
  • snowflake-watumiaji

Hatimae,anza tena Tor Browser. Hii inapashwa kurekebisha masuala uliyokumbana nayo. tafadhari kumbuka kwamba wateja wa antivirus, kama Kaspersky, pia anatakiwa afungiwe Tor katika nafasi ya firewall.