Kwa asili yake, mteja wako wa Tor anasikiliza tu applikesheni ambazo zimeunganishwa na mendeshaji wa ndani. Mawasiliano na kompyuta nyingine zimekataliwa. Kama unataka kutumia aplikesheni kwenye kompyuta nyingi kuliko mteja wa Tor, unaweza kuhariri torrc zako kuelezea anwani ya SocksListern 0.0.0.0 pia anzisha upya Tor. Kama unataka kupata iliyo bora zaidi, unaweza kusanidi mteja wako wa Tor ulinzi imara kujenga anwani yako ya IP ya ndani na sio anwani yako ya nje ya IP.