Tor Browser inafanya muunganiko wako ujitokeze japo hutoka kwenye sehemu tofauti za dunia. Baadhi ya tovuti, kama vile bank au watoa huduma za email, wanaweza kutasfiri kuwa alama hii ni akaunti yako imeondolewa na kukufungia.

Njia pekee ya kutatua hili ni kufuata mapendekezo ya utaratibu wa tovuti ili kurejesha akunti au kuwasiliana na waeneshaji na uwaelezee hali hiyo.

Unaweza kuzuia hali hii kama mtoa huduma wako ametoa uthibitishaji wa awamu ya pili, ambayo ni ulinzi bora kuliko zifa za msingi za IP. Mtafute mtoa huduma wako na wauulize kama wanatoa 2A.