Unapotumia Tor Browser wakati mwingine inaweza kuwa taratibu kuliko kivinjari kingine. Mtandao wa Tor una watumiaji wa kila siku zaidi ya milioni, na zaidi ya ralays 6000 kwa ajili ya kusafirisha data zoite, na mzigo katika kila seva unaweza kusababisha ucheleshwaji. Na, kwa muundo, usafirishaji wako unaruka kwa kupitia seva za wanajitolea katika vifaa mbalimbali duniani, na kwa kawaida baadhi ya vikwazo na ucheleshwaji utakuwepo. Unaweza kusaidia kuborewsha kasi ya mtandao kwa running your own relay, au kuhamasisha wengine kufanya hivyo. Kwa majibu ya kina zaidi, angaliaChapisho la blogu la Roger kuhusu mada na Mada za Tor's Open Research: toleo la 2018 kuhusu Utendaji wa Mtandao. Unaweza pia kuangalia chapisho letu la hivi majuzi la blogu Ulinzi wa mtandao wa Tor dhidi ya Mashambulizi Yanayoendelea, ambalo linajadili mashambulizi ya Kunyimwa Huduma (DoS) kwenye Tor Mtandao. Zaidi ya hayo, tumeanzisha Ulinzi wa Uthibitisho wa Kazi kwa Huduma za Onion ili kusaidia kupunguza baadhi ya mashambulizi haya. Kusema hivyo, Tor ni ya haraka zadi ya ilivyokuwa mwanzo na unaweza usigundue tofauti yoyote katika kasi ukilinganisha na vkivinjari kingine.