Ikiwa muunganisho wako wa intaneti unaweza kuwa unazuia mtandao wa Tor, unaweza kujaribu kutumia viungo. Baadhi ya viungo vimejengwa katika Kivinjari cha Tor na vinahitaji hatua chache kuwezesha. Kutumia pluggable transport, bofya "Configure Connection" unapoanza kutumia Tor Browser kwa mara ya kwanza. Chini ya sehemu ya "Bridges", onyesha chaguo la "Choose from one of Tor Browser's built-in bridges" na bofya katika chaguo la "Select a Built-In Bridge". Kutoka katika mpangilio, chagua chochote pluggable transport utakachopenda kukitumia.

Pale unapokuwa umechagua pluggable transport, pandisha juu na bofya "Connect" kuhifadhi mpangilio.

Au, kama unatumia Tor Browser, Bonyeza "Settings" katika menu iliyofichwa (≡) na halafu "Connection" katika ubao wa pembeni. Chini ya sehemu ya "Bridges", onyesha chaguo la "Choose from one of Tor Browser's built-in bridges" na bofya katika chaguo la "Select a Built-In Bridge". Chagua pluggable transport wowote ungependa kutumia kutoka katika muongozo. Mpangilio wako utahifadhiwa otomatiki pale tu utakapofunga kurasa.

Ikiwa unahitaji bridges nyingine, unaweza kupata katika Bridges website yetu. Kwa taarifa zaidi kuhusu bridges, angalia Tor Browser manual.