Udhibiti

Ikiwa huwezi kupakua Kivinjari cha Tor kupitia tovuti, unaweza kupata nakala ya Kivinjari cha Tor utakayoipokea kupitia GetTor. GetTor ni huduma ya kiotomatiki inayojibu ujumbe katika anwani katika toleo jipya la Tor Browser, zinazomilikiwa katika maeneo mbalimbali ambayo yana uwezekano mdogo wa kudhibitiwa, kama vile Dropbox, Google Drive, na GitHub. Unaweza kuiomba kupitia Barua pepe or Telegram bot https://t.me/gettor_bot. Unaweza pia kupakua Tor Browser kutoka https://tor.eff.org or from https://tor.calyxinstitute.org/.

Tuma barua pepe kwenda gettor@torproject.org Katika ujumbe wa barua pepe, andika jina la mfumo wa uendeshaji (kama vile Windows, macOS, au Linux). GetTor itajibu kwa barua pepe iliyo na anwani unayoweza kupakua Tor Browser, sahihi ya picha (itahitajika kuthibitisha upakuaji), fingerprint ya funguo iliyotumika kuwekea sahihi, na kifurushi cha checksum. Unaweza kupewa chaguo la programu ya "32-bit" au "64-bit": hii itategemea na aina ya kompyuta unayotumia, angalia nyaraka kuhusu kompyuta yako ili kujua zaidi.

Ikiwa unashuku kuwa serikali yako au Mtoa Huduma za Intaneti (ISP) ametekeleza aina fulani ya udhibiti wa Intaneti au uchujaji, unaweza kujaribu kama mtandao wa Tor unazuiwa kwa kutumia OONI Probe. OONI Probe ni programu ya bure na programu ya open source iliyotengenezwa na Open Observatory of Network Interference (OONI). Imeundwa ili kujaribu na kupima tovuti, programu za kutuma ujumbe na zana za kukwepa ambazo zinaweza kuzuiwa.

Kabla ya kuendesha majaribio haya ya vipimo, tafadhali soma kwa makini mapendekezo ya usalama ya OONI na tathmini ya hatari. Kama zana nyingine yoyote ya majaribio, tafadhali fahamu majaribio chanya cha uwongo OONI.

li kuangalia kama Tor imezuiwa, unaweza kusakinisha OONI Probe kwenye kifaa chako cha mkononi au kwenye eneo-kazi lako, na kuendesha "Circumvention Test". Jaribio la Tor la OONI linaweza kutumika kama kielelezo cha kizuizi kinachowezekana cha mtandao wa Tor, lakini uchambuzi wa kina wa wasanidi wetu ni muhimu kwa tathmini ya mwisho.

Tor Browser inaweza kwa uhakika kuwasaidia watu kufika tovuti yako katika sehemu ambazo zimezuiliwa. Mara nyingi, Pakua kwa urahisi Tor Browser na uitumie kutafuta tovuti zilizozuiliwa ili kuruhusu kufikiwa. Katika maeneo yenye udhibiti mkali tuna machaguo kadhaa ya kukwepa udhibiti huo, ikiwemo pluggable transports.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali angalia Tor Browser User Manual section on censorship circumvention.

Kama unapata changamoto katika kuunganisha, ujumbe wa dosari unaweza kutokea na unaweza kiuchagua "copy Tor log to clipboard". Kisha nakili matatizo ya Tor log katika faili la kipimo au nyaraka nyingine.

Ikiwa hutaona chaguo na Tor Browser ikiwa inafanya kazi, unaweza kuingia katika hamburger menu ("≡"), halafu bonyeza "settings", na mwishoni "Connection" katika apande wa pembeni. Chini katika kurasa, pembeni ya maandishi ya "View the Tor logs", bofya kitufe cha "View Logs...".

Njia mbadala, katika GNU/Linux, kuona tatizo hapohapo katika kifaa, peruzi katika saraka ya Tor Browserna ianzishe kutumia Tor Browser kutoka katika sehemu ya amri:

./start-tor-browser.desktop --verbose

au kutunza kumbukumbu katika faili (default: tor-browser.log)

./start-tor-browser.desktop --log [file]

Utapaswa kuona mojawapo ya makosa katika kumbukumbu za kawaida (angalia mistari ifuatayo katika kumbukumbu zako za Tor):

Kumbukumbu ya hitilafu ya kawaida #1: Kushindwa kwa muunganiko wa Proxy

2017-10-29 09:23:40.800 [NOTICE] Opening Socks listener on 127.0.0.1:9150
2017-10-29 09:23:47.900 [NOTICE] Bootstrapped 5%: Connecting to directory server
2017-10-29 09:23:47.900 [NOTICE] Bootstrapped 10%: Finishing handshake with directory server
2017-10-29 09:24:08.900 [WARN] Proxy Client: unable to connect to xx..xxx..xxx.xx:xxxxx ("general SOCKS server failure")

Ikiwa utaona mistari kama hii katika kumbukumbu za Tor, hii inamaanisha zinashindwa kuunganishwa katika SOCKS proxy. Ikiwa SOCKS proxy itahitajika katika mapngilio wa mtandao wako, basi tafadhali hakikisha kuwa umeingiza maelezo yako katika proxy kwa usahihi. Ikiwa SOCKS proxy haihitajiki, au hauna uhakika, tafadhari jaribu kuunganisha mtandao wa Tor bila kutumia SOCKS proxy.

Kumbukumbu la kosa la kawaida #2. Haifikii guard relays

11/1/2017 21:11:43 PM.500 [NOTICE] Opening Socks listener on 127.0.0.1:9150
11/1/2017 21:11:44 PM.300 [NOTICE] Bootstrapped 80%: Connecting to the Tor network
11/1/2017 21:11:44 PM.300 [WARN] Failed to find node for hop 0 of our path. Discarding this circuit.
11/1/2017 21:11:44 PM.500 [NOTICE] Bootstrapped 85%: Finishing handshake with first hop
11/1/2017 21:11:45 PM.300 [WARN] Failed to find node for hop 0 of our path. Discarding this circuit.

Ikiwa utaona mistari kama hii katika kumbukumbu za Tor, hii inamanisha Tor imeshindwa kuunganisha node ya kwanza katika Tor circuit. Hii inaweza kumaanisha kuwa upo katika mtandao uliodhibitiwa.

Tafadhari jaribu kuunganisha kupitia bridges, na baada ya hapo inapaswa kurekebisha tatizo.

Kumbukumbu la kosa la kawaida #3; Imeshindwa kukamilisha TLS handshake

13-11-17 19:52:24.300 [NOTICE] Bootstrapped 10%: Finishing handshake with directory server 
13-11-17 19:53:49.300 [WARN] Problem bootstrapping. Stuck at 10%: Finishing handshake with directory server. (DONE; DONE; count 10; recommendation warn; host [host] at xxx.xxx.xxx.xx:xxx) 
13-11-17 19:53:49.300 [WARN] 10 connections have failed: 
13-11-17 19:53:49.300 [WARN]  9 connections died in state handshaking (TLS) with SSL state SSLv2/v3 read server hello A in HANDSHAKE 
13-11-17 19:53:49.300 [WARN]  1 connections died in state connect()ing with SSL state (No SSL object)

Ikiwa utaona mistari hii katika kumbukumbu za Tor, hii inamaanisha Tor imeshinda kumalizia TLS handshake katika directory. Kutumia madaraja inaweza kurekebisha hii.

Kumbukumbu la kosa la kawaida #4: Clock skew

19.11.2017 00:04:47.400 [NOTICE] Opening Socks listener on 127.0.0.1:9150 
19.11.2017 00:04:48.000 [NOTICE] Bootstrapped 5%: Connecting to directory server 
19.11.2017 00:04:48.200 [NOTICE] Bootstrapped 10%: Finishing handshake with directory server 
19.11.2017 00:04:48.800 [WARN] Received NETINFO cell with skewed time (OR:xxx.xx.x.xx:xxxx): It seems that our clock is behind by 1 days, 0 hours, 1 minutes, or that theirs is ahead. Tor requires an accurate clock to work: please check your time, timezone, and date settings.

Ikiwa utaona mistari hii katika kumbukumbu za Tor, hii inamaanisha mfumo wako wa saa haupo sahihi. Tafadhari hakikisha saa yako imewekwa sahihi, ikiwemo usahihi wa majira ya ukanda, Halafu anzisha tena Tor.

Relays za Bridge ni relays za Tor ambazo hazitaorodheshwa katika umma ya sakara ya Tor.

Hii inamaanisha kuwa watoa huduma za mtandao au serikali wakijaribu kuzia kufikiwa kwa mtandao wa Tor hawawezi kuzuia bridge zote. Bridges hufaa kwa watumiaji wa Tor bila sheria, na kwa watu wanaohitaji tabaka za ziada la ulinzi sababu wanahofia mtu anaweza kuwatambua kuwa wanawasiliana kutumia anwani ya IP ya Tor relay.

Bridge ni relay ya kawaida tu yenye usanidi wa kiutofauti kidogo. Angalia How do I run a bridge kwa maelekezo.

Nchi mbalimbali, Ikiwemo China na Iran, zimetafuta njia kugundua kuzuiwa kwa muunganishwa wa Tor bridges. Obfsproxy bridges zinashughulikia haya kwa kuongeza tabaka lingine la utafutaji. Kupangilia obfsproxy bridge kunahitaji kifurushi cha ziada cha programu na nyongeza ya usanidi. Angalia katika kurasa yetu pluggable transports Kwa taarifa zaidi.

Snowflake ni pluggable transport unaopatikana katika Tor Browser katika kugundua udhibiti wa mtandao. Kama Tor bridge, mtumiaji anaweza kupata mtandao uliachiwa wakati hata kama muunganisho wa kawaida wa Tor umedhibitiwa. Kutumia Snowflake ni rahisi kama kubadili usanidi wa bridge mpya katika Tor Browser.

Mfumo huu unajumuisha vipengele vitatu: Watu wanaojitolea kuendesha proxies za Snowflake, Watumiaji wa Tor wanaotaka kuunganishwa kwenye mtandao, na wakala, ambaye hutoa proxies Snowflake kwa watumiaji.

Watu wanaojitolea wapo tayari kuwasaidi watumiaji katika udhibiti wa mtandao wanaweza kuwasaidia kwa kusokota short-lived proxies katika browser zao za kawaida, Angalia, how can I use Snowflake?

Snowflake hutumia mbinu yenye ufanisi mkubwa domain fronting kufanya muunganisho kwa mojawapo ya maelfu ya proxies za snowflake zinazoendeshwa na watu wanaojitolea. Proxies hizi ni nyepesi, za muda mfupi, na rahisi kuzitumia, zinazoturuhusu kupima Snowflake kwa urahisi zaidi kuliko mbinu za kizamani.

Kwa watumiaji waliodhibitiwa, Kama Snowflake yako imezuiwa, mzuiaji atatafuta proxy mpya kwa ajili yako, kiotomatiki.

Kama unavutiwa na maelezo za kiufundi na kujua sifa zake, angalia Snowflake Technical Overview and the project page. Kwa mazungumzo mengine kuhusu Snowflake, tafadhari tembelea Tor Forum na fuatilia Snowflake tag.

Snowflake inapatikana katika Tor Browser majukwaa mahiri: Windows, macOs, GNU/Linux, na Android. Unaweza kutumia pia Snowflake katika Onion Browser katika iOS.

Ukiwa unatumia Tor Browser katika kompyuta ya mezani kwa mara ya kwanza bonyeza "Sanidi muunganisho" katika kioo cha mbele cha kifaa unachotumia. Chini ya sehemu ya "Bridges", onyesha chaguo la "Choose from one of Tor Browser's built-in bridges" na bofya katika chaguo la "Select a Built-In Bridge". Kutoka katika mpangilio, Chagua 'Snowflake'. Mara tu unapochagua Snowflake, pandisha juu na bonyeza 'Connect' ili kuhifadhi mpangilio.

Kutoka ndani ya browser, unaweza kubonyeza katika hamburger menu ("≡"), halafu nenda kwenye 'Settings" na halafu nenda 'Connection'. Mbadala, unaweza pia kuandika about:preferences#connection sehemu ya kuandikia URL. Chini ya sehemu ya "Bridges", onyesha chaguo la "Choose from one of Tor Browser's built-in bridges" na bofya katika chaguo la "Select a Built-In Bridge". Kutoka katika mpangilio, Chagua 'Snowflake'.

Ikiwa upatikaji wako wa mtandao haujadhibitiwa, unapaswa kuzingatia kusanikisha na kuboresha Snowflake ili kuwasaidia watumiaji katika udhibiti wa mtandao. Unapoendesha Snowflake kwenye kivinjari chako cha kawaida, utakuwa na proksi ya trafiki kati ya watumiaji waliodhibitiwa na nodi ya kuingia kwenye mtandao wa Tor na hiyo ndiyo yote.

Kwa sababu ya udhibiti wa seva za VPN katika baadhi ya nchi tunakuomba usiendeshe proksi ya snowflake wakati umeunganishwa kwenye VPN.

Ongeza-katika

Kwanza hakikisha unawezesha WebRTC. Halafu unaweza kusanikisha hii uenezi wa Firefox au uenezi wa Chrome ambayo itakufanya wewe kuwa Snowflake proxy. Pia inaweza kukutaarifu kuhusu watu wangapi uliwasaidi katika masaa 24 yaliyopita.

Kurasa ya tovuti

Katika browser ambapo WebRTC imewezeshwa: Kama hutaki kuongeza Snowflake katika browser yako, unaweza kuingia katika https://snowflake.torproject.org/embed na ugeuze kitufe ili kuchagua kuingia kuwa proxy. Huwezi kufunga kurasa kama unataka kubakiza Snowflake proxy.

Ikiwa muunganisho wako wa intaneti unaweza kuwa unazuia mtandao wa Tor, unaweza kujaribu kutumia viungo. Baadhi ya viungo vimejengwa katika Kivinjari cha Tor na vinahitaji hatua chache kuwezesha. Kutumia pluggable transport, bofya "Configure Connection" unapoanza kutumia Tor Browser kwa mara ya kwanza. Chini ya sehemu ya "Bridges", onyesha chaguo la "Choose from one of Tor Browser's built-in bridges" na bofya katika chaguo la "Select a Built-In Bridge". Kutoka katika mpangilio, chagua chochote pluggable transport utakachopenda kukitumia.

Pale unapokuwa umechagua pluggable transport, pandisha juu na bofya "Connect" kuhifadhi mpangilio.

Au, kama unatumia Tor Browser, Bonyeza "Settings" katika menu iliyofichwa (≡) na halafu "Connection" katika ubao wa pembeni. Chini ya sehemu ya "Bridges", onyesha chaguo la "Choose from one of Tor Browser's built-in bridges" na bofya katika chaguo la "Select a Built-In Bridge". Chagua pluggable transport wowote ungependa kutumia kutoka katika muongozo. Mpangilio wako utahifadhiwa otomatiki pale tu utakapofunga kurasa.

Ikiwa unahitaji bridges nyingine, unaweza kupata katika Bridges website yetu. Kwa taarifa zaidi kuhusu bridges, angalia Tor Browser manual.

Watumiaji wa nchini Chini wanahitaji kuchukua hatua chache za kudhibiti Great Firewall na kujiunganisha katika mtandao wa Tor.

Kupata toleo lililosasishwa la Tor Browser, Jaribu mtandao wa Telegram kwanza: https://t.me/gettor_bot. Ikiwa haifanyi kazi, unaweza kutuma barua pepe katika gettor@torproject.org kikiwa na kichwa cha habari "windows", "macos", au "linux" kutokana na mfumo wa uendeshaji husika.

Baada ya kusanikisha, Tor Browser itajaribu kuunganisha katika mtandao wa Tor. Ikiwa Tor imedhibitiwa eneo lako, Connection Assist itajaribu kuunganishwa otomatiki kwa kutumia bridge au Snowflake. Lakini kama haitafanya kazi, hatua ya pili itaweza kupata bridge inayofanya kazi nchini China.

Kuna machaguo matatu ya kutoa kuzuiliwa kwa Tor nchini China:

  1. Snowflake: hutumia ephemeral proxies kuunganishwa kwenye mtandao wa Tor. Inapatikana katika Tor Browser na Tor programu nyingine zinazoendeshwa kama Orbot. Unaweza kuchagua Snowflake kutoka Tor Browser's built-in bridge menu.
  2. Private and unlisted obfs4 bridges: huwasiliana na Telegram @GetBridgesBot and type /bridges. Au tuma barua pepe kwendafrontdesk@torproject.org ikiwa na maneno "private bridge cn" katika kichwa cha habari. Kama wewe tech-savvy, unaweza kuendesha obfs4 bridge yetu nje ya nchi ya China. Kumbuka kuwa bridges yanasambazwa na BridgeDB, na kuundwa katika obfs4 yaliyounganishwa katika Tor browser yenye uwezekano mkubwa wa kutokufanya kazi.
  3. meek-azure: inafanya ionekane kana una browsing tovuti ya Microsoft badala ya kutumia Tor. Hata hivyo, kwa sababu ina kizuizi cha kiwango cha mwisho, chaguo hili litakuwa taratibu. Unaweza kuchagua meek-azure kutoka Tor Browser's built-in bridges dropdown.

Ikiwa moja ya machaguo haya juu hayafanyi kazi, angalia Tor logs yako na jaribu chaguo lingine.

Kama unahitaji msaada, pia utapata msaada katika Telegram https://t.me/TorProjectSupportBot and Signal.

Pata maagizo ya kisasa kuhusu jinsi ya kukwepa udhibiti na kuunganisha kwa Tor kutoka Urusi kwenye mwongozo wetu wa jukwaa : Tor imezuiwa nchini Urusi - jinsi ya kukwepa udhibiti.

Ikiwa unahitaji msaada, wasiliana nasi kupitia Telegramu, WhatsApp, Signal, au kwa barua pepe frontdesk@torproject.org. Kwa maagizo ya kukwepa udhibiti, tumia "private bridge ru" kama mada ya barua pepe yako.

kunawakati tovuti itafunga watumiaji wa Tor kwasababu haziwez kuonesha tofauti kati ya usawa wa mtumiaji wa Tor na trafic ya kiautomatiki. Kwa mafanikio mazuri ni kupata ukurasa kwa watumiaji kuifungua Tor watumiaji watapata kuwasiliana na wasimamizi wa tovuti moja kwa moja. Kitu kama hiki inaweza kuwa ni ujanja:

"Habari!" nimejaribu kuifikia tovuti yako xyz.com huku nikitumia Tor Browser na nimegundua kwamba hujawaruhusu watumiaji wa Tor kuifikia tovuti yako. Nakuhimiza kuzingatia maamuzi haya: Tor hutumika na watu duniani kote kulinda faragha zao na kupinga udhibiti. Kwa kudhibiti watumiaji wa Tor, ni kama umewadhibiti watu katika nchi zao ambao wanataka kutumia mtandao wa bure, waandishi wa habari, watafiti ambao wanataka kujilinda wenyewe dhidi ya ugundunduzi, watoa taarifa, wanaharakati na watu wakawaida ambao wanataka kujiondoa kwenye wadukuzi. Tafadhali chukua msimamo mkali kwa kuzingatia faragha za kidigitali na uhuru wa mtandao na ruhusu watumiaji wa Tor kupata xyz.com. Ahsante"

Kwa kesi za bank, na tovuti nyingine muhimu, ni kawaida kuona udhibiti wa msingi wa jiografia (kama bank imejua umeweza kupata huduma zao kutoka nchi moja, na ghafla umejiunganisha na exit relay kwenye upande mwingine wa dunia, akaunti yako inaweza kudhibitiwa au kuondolewa).

Kama umeshindwa kujuinganisha na onion services, tafadhali tazama siwezi kuipata X.onion!.