Watumiaji wa nchini Chini wanahitaji kuchukua hatua chache za kudhibiti Great Firewall na kujiunganisha katika mtandao wa Tor.

Kupata toleo lililosasishwa la Tor Browser, Jaribu mtandao wa Telegram kwanza: https://t.me/gettor_bot. Ikiwa haifanyi kazi, unaweza kutuma barua pepe katika gettor@torproject.org kikiwa na kichwa cha habari "windows", "macos", au "linux" kutokana na mfumo wa uendeshaji husika.

Baada ya kusanikisha, Tor Browser itajaribu kuunganisha katika mtandao wa Tor. Ikiwa Tor imedhibitiwa eneo lako, Connection Assist itajaribu kuunganishwa otomatiki kwa kutumia bridge au Snowflake. Lakini kama haitafanya kazi, hatua ya pili itaweza kupata bridge inayofanya kazi nchini China.

Kuna machaguo matatu ya kutoa kuzuiliwa kwa Tor nchini China:

  1. Snowflake: hutumia ephemeral proxies kuunganishwa kwenye mtandao wa Tor. Inapatikana katika Tor Browser na Tor programu nyingine zinazoendeshwa kama Orbot. Unaweza kuchagua Snowflake kutoka Tor Browser's built-in bridge menu.
  2. Private and unlisted obfs4 bridges: huwasiliana na Telegram @GetBridgesBot and type /bridges. Au tuma barua pepe kwendafrontdesk@torproject.org ikiwa na maneno "private bridge cn" katika kichwa cha habari. Kama wewe tech-savvy, unaweza kuendesha obfs4 bridge yetu nje ya nchi ya China. Kumbuka kuwa bridges yanasambazwa na BridgeDB, na kuundwa katika obfs4 yaliyounganishwa katika Tor browser yenye uwezekano mkubwa wa kutokufanya kazi.
  3. meek-azure: inafanya ionekane kana una browsing tovuti ya Microsoft badala ya kutumia Tor. Hata hivyo, kwa sababu ina kizuizi cha kiwango cha mwisho, chaguo hili litakuwa taratibu. Unaweza kuchagua meek-azure kutoka Tor Browser's built-in bridges dropdown.

Ikiwa moja ya machaguo haya juu hayafanyi kazi, angalia Tor logs yako na jaribu chaguo lingine.

Kama unahitaji msaada, pia utapata msaada katika Telegram https://t.me/TorProjectSupportBot and Signal.