Snowflake inapatikana katika Tor Browser majukwaa mahiri: Windows, macOs, GNU/Linux, na Android. Unaweza kutumia pia Snowflake katika Onion Browser katika iOS.

Ukiwa unatumia Tor Browser katika kompyuta ya mezani kwa mara ya kwanza bonyeza "Sanidi muunganisho" katika kioo cha mbele cha kifaa unachotumia. Chini ya sehemu ya "Bridges", onyesha chaguo la "Choose from one of Tor Browser's built-in bridges" na bofya katika chaguo la "Select a Built-In Bridge". Kutoka katika mpangilio, Chagua 'Snowflake'. Mara tu unapochagua Snowflake, pandisha juu na bonyeza 'Connect' ili kuhifadhi mpangilio.

Kutoka ndani ya browser, unaweza kubonyeza katika hamburger menu ("≡"), halafu nenda kwenye 'Settings" na halafu nenda 'Connection'. Mbadala, unaweza pia kuandika about:preferences#connection sehemu ya kuandikia URL. Chini ya sehemu ya "Bridges", onyesha chaguo la "Choose from one of Tor Browser's built-in bridges" na bofya katika chaguo la "Select a Built-In Bridge". Kutoka katika mpangilio, Chagua 'Snowflake'.