Ikiwa unashuku kuwa serikali yako au Mtoa Huduma za Intaneti (ISP) ametekeleza aina fulani ya udhibiti wa Intaneti au uchujaji, unaweza kujaribu kama mtandao wa Tor unazuiwa kwa kutumia OONI Probe. OONI Probe ni programu ya bure na programu ya open source iliyotengenezwa na Open Observatory of Network Interference (OONI). Imeundwa ili kujaribu na kupima tovuti, programu za kutuma ujumbe na zana za kukwepa ambazo zinaweza kuzuiwa.

Kabla ya kuendesha majaribio haya ya vipimo, tafadhali soma kwa makini mapendekezo ya usalama ya OONI na tathmini ya hatari. Kama zana nyingine yoyote ya majaribio, tafadhali fahamu majaribio chanya cha uwongo OONI.

li kuangalia kama Tor imezuiwa, unaweza kusakinisha OONI Probe kwenye kifaa chako cha mkononi au kwenye eneo-kazi lako, na kuendesha "Circumvention Test". Jaribio la Tor la OONI linaweza kutumika kama kielelezo cha kizuizi kinachowezekana cha mtandao wa Tor, lakini uchambuzi wa kina wa wasanidi wetu ni muhimu kwa tathmini ya mwisho.