Unapokuwa na Tor Browser wazi unaweza kuperuzi katika hamburger menu ("≡"), kisha bofya katika "Settings", na mwisho katika "Connection" upande wa pembeni. Chini katika kurasa, pembeni ya maandishi ya "View the Tor logs", bofya kitufe cha "View Logs...". Unatakiwa kuona chaguo la kunakili historia yako katika kurasa yako, amabayo utakuwa na uwezo wa kunakilisha katika ukurasa wa kuandikia au kutuma barua pepe kwa mtumiaji.

Njia mbadala, katika GNU/Linux, kuona tatizo hapohapo katika kifaa, peruzi katika saraka ya Tor Browserna ianzishe kutumia Tor Browser kutoka katika sehemu ya amri:

./start-tor-browser.desktop --verbose

au kutunza kumbukumbu katika faili (default: tor-browser.log)

./start-tor-browser.desktop --log [file]