Google hutumia "eneo la kijographia" kutambua upo wapi duniani, hivyo inaweza kukupa uzoefu binafsi. Hii huusisha utumiaji wa lugha inadhani unapendelea, pia inahusisha kukupa matokeo tofauti ya maswali yako.

Kama unataka kuonga Google kwa lugha ya kiingereza unweza kugusa link ambayo inatoa lugha hiyo. Lakini tunazingatia sifa za Tor, na sio tatizo--- Mtandao sio tambarare, na kiuhalisia huonekana tofauti inategemea na wapi ulipo. Sifa hizi hukumbusha watu kuhusu hili.

Zingatia URL za Google search huchukua jina/ thamani ya jozi za hoja na moja ya majina hayo ni "hl". Kama unatuma "hl" kwenda "en" ndipo Google watakurudishia matokea kwa lugha ya kiingereza bila kujali ni Google seva ipi umetuma. Link iliyobadilika inaweza kuonekana kama hivi:

https://encrypted.google.com/search?q=online%20anonymity&hl=en

Mbinu nyingine ni kurahisisha msimbo wa nchi yako ili kupata Google. Hii inaweza kuwa google.be, google.de, google.us na nyinginezo.