Historia ya uperuzi wa Tor Browser pekee itakwenda kwenye mtandao wa Tor. Applikesheni nyingine yeyote kwenye mfumo wako (ikiwemo browser nyingine) haitakuwa na mawasiliano katika mtandao wa To, na haitakuwa na ulinzi. Unatakiwa kusanidiwa tofauti kutumia Tor. Kama unahitaji kuwa na uhakika kuwa trafiki yote itakwenda kwenye mtandao wa Tor, tazama mfumo wa uendeshaji wa moja kwa moja wa Tails ambao unaweza kuanza kwenye kompyuta yeyote kutoka kwenye USB au DVD.