Tunasanidi NoScript kuruhusu JavaScript kwa asili yake katika Tor Browser kwa sababu tovuti nyingi hazitafanya kazi na JavaScript zilizoshindwa kufanya kazi. Watumiaji wengi, watakata tamaa na Tor kama hatutawezesha JavaScript kwa asili yake kwa sababu itasababisha matatizo mengi kwao. Hatimaye, tunataka kufanya Tor Browser iwe salama kadri iwezekanavyo huku ukiendelea kutumika na watu wengi, kwa sasa, inamaanisha kuondoa JavaScript inawezeshwa kwa asili yake.

Kwa watumiaji wanotaka kuwa na JavaScript isiyofanyekazi katika tovuti zote za HTTP kwa asili yake, tunapendekeza badilisha "kiwango cha ulinzi" katika Tor Browser yako. Hii inaweza kufanywa kwa kusafirisha alama ya ulinzi (ngao ndogo ya kijivu kwenye sehemu ya juu ya kulia ya kioo), kisha bonyeza "Change...". "Kiwango cha kawaida" uruhusu JavaScript, kiwango "salama" uzuia JavaScript kwenye tovuti za HTTP na kiwango salama zaidi huzuia JavaScript zote pamoja.