Tor Browser kwa sasa inapatikana kwenye Windows, Linux, macOS na Android.

Kwenye Android, Mradi wa Guardian pia hutoa programu ya Orbot kuelekeza programu zingine kwenye kifaa chako cha Android kupitia mtandao wa Tor.

Hakuna toleo rasmi la Kivinjari cha Tor kwa iOS bado, kama ilivyoelezwa katika chapisho hili la blogu. Pendekezo letu bora linalopatikana ni Kivinjari cha Onion.