Kama unatumia Tor Browser na kivinjari kingine kwa wakati mmoja, haita athili utendaji wa Tor au tabia ya faragha.

Hatahivyo, jua kwamba unapotumia Tor na kivinjari kingine kwa wakati mmoja, shughuli zako za Tor zinaweza kuingiliana na shughuli zisizo za Tor (halisi) IP kutoka katika kivinjari kingine, kwa kusogeza mausi yako toka katika kivinjari kimoja kwenda kingine.

Au unaweza kusahau kwa bahati mbaya ukatumia kivinjari kisicho na faragha kufanya jambo fulani ambacho umekusudia kufanya katika Tor Browser badala yake.