hapana, Tor Browser ni programu huria na ni bure. kivinjari chochote kinachokulazimisha kulipia na inadai kuwa Tor Browser ni feki. Ili kuhakikisha kuwa unapakua kivinjari sahihi cha Tor Browser tembelea ukurasa wetu wa kupakua kwa kubofya hapa:download page. Baada ya kupakua, unaweza kuhakikisha kuwa una toleo rasmi la Tor Browser kwa kuthibitisha saini. Kama unashindwa kufungua tovuti yetu. tembelea censorship section]kupata habari kuhusu njia mbadala ya kupakua Tor Browser.

Ikiwa umelipia programu ghushi inayodai kuwa Kivinjari cha Tor, unaweza kujaribu kuomba kurejeshewa pesa kutoka kwa Apple au Play Store au unaweza kuwasiliana na benki yako ili kuripoti shughuli ya ulaghai. Hatuwezi kukurejeshea pesa kwa ununuzi uliofanywa kwa kampuni nyingine.

Unaweza kutoa taarifa kwa Tor Browser feki kwenye frontdesk@torproject.org