Tor Browser ni toleo lililo boreshwa la Firefox hususani imeundwa kwa matumizi na Tor. Kazi kubwa zimefanyika kuifanya Kivinajri chaTor, ikijumuisha utumiaji wa patch za ziada kuimarisha faragha na ulinzi. Kiufundi inawezekana kutumia Tor pamoja na vivinjari vingine, unaweza ukajiweka katika uwezekano wa kushambuliwa au kuvuja kwa taarifa, hivyo tunawakatisha tamaa kwa hilo. Jifunze zaidi kuhsu muundo wa Tor Browser.