Kila tunapotoa tolea jipya laf Tor Browser iliyo imara, tuaandika chapisho la blogi lenye maelezo kuhusiana nayo na vipengere na sifa mpya zilizopo na matatiozo yanayofahamika. Kama umeanza kupata matatizo katika Tor Browser yako baada ya kusasisha, angalia blog.torproject.org kwa ajili ya chapisho lihusulo Tor Browser imara ya hivi karibuni kuona kama tatizo lako limeorodheshwa. Kama tatizo lako halijaorodheshwa huko, tafadhali kwanza angalia Tor Browser's issue tracker na tengeneza GitLab issue kuhusiana na ulichokutana nacho.