Huku majina yanaweza yakaashiria, 'muundo wa Incognito' na 'tab za faragha' haifanyi ujulikane kwenye mtandao.
Wanaondoa taarifa zote kwenye mashine inayohusiana na kipengele cha kuperuzi baada ya kufunga, lakini hakuna mbinu za kuficha shughuli zako au alama zako za kidigitali mtandaoni.
Hii humaanisha kuwa mtazamaji anaweza kukusanya uperuzi wako kwa urahisi kwenye browser yeyote.
Tor Bowser hutoa sifa zote za tab za faragha huku zikificha chanzo cha IP, mazoea ya kuperuzi na taarifa kuhusu kifaa ambacho kinaweza kutumika kama alama shughuli kwenye tovuti, kuruhusu uperuzi binafsi wa kweli ambayo imesimbwa .
Kwa taarifa zaidi juu ya vizuizi vya muundo wa Incognito na tab binafsi, tazama makala ya Mozilla kwenye Hadithi za kawaida kuhusu kuperuzi kwa faragha.