Ndio.

Programu ya Tor ni programu isiyoitaji garama. Hii inamaanisha tunakupatia haki ya kusambaza programu ya Tor, aidha iliyorekebishwa au isiyorekebishwa, aidha kwa kulipia au bure. Hauhitaji kutuomba ruhusa maalum.

Japokuwa, kama unataka kuzirudia kusambaza programu za Tor unatakiwa kufuata leseni. Kimsingi hii inamaanisha kwamba unatakiwa kulihusisha faili la leseni kwenye sehemu yeyote ya programu ya Tor unayosambaza.

Watu wengi ambao wanatuuliza swali hili ingawa hawataki kusambaza programu ya Tor. Wanataka kusambaza kivinjari cha Tor. Hii hujumuisha Toleo la usaidizi la Firefoxna ugani la NoScript. Utatakiwa kufuata leseni kwa proggramu zote vivyo hivyo. Viendelezi vyote vya Firefox vimesambazwa chini ya, GNU General Public License huku Firefox ESR imetolewa chini ya leseni ya umma ya Mozilla. Namna rahisi ya kutii leseni zao ni kujumuisa msimbo wa chanzo kwa programu hizi popote utakapo jumuisha vifurushi vyenyewe.

Pia, unatakiwa kuhakikisha huwachanganyi wasomaji wako kuhusu Tor ni nini, nani aliyeitengeneza na inatoa vitu gani (na isivyotoa). Angalia alama yetu ya biashara FAQ kwa taarifa zaidi.