Kama unatumia Tor relay ambayo inakuruhusu kujitoa kwenye muunganiki (kama vile sera za kujitoa kiotomatiki), pengine ni salama kusema kuwa mwishowe utasikia kwa mtu fulani. Malalamiko ya unyanyasaji yanaweza kuja na namna nyingi. Kwa mfano:

  • Mtu mmoja alijiunganisha na Hotmail, na akatuma fidia kwa kampuni. FBI wamekutumia barua pepe ya heshima, uelezee kwamba umetumia relay za Tor, na wanasema ""oh vizuri" na kukuacha.[Port 80]
  • Mtu mmoja anajaribu kukushusha kwa kutumia Tor kuunganisha makundi ya Google na kuchapisha taarifa za uzushi katika mtandao, na anatuma barua pepe ya hasira kwa ISP wako kuhusu namna ulivyoharibu dunia. [Port 80]
  • Mtu mmoja alijiungganisha na mtandao wa IRC na akaijtengenezea kosa. ISP wako atapata barua pepe ya heshima kuhusu namna kompyuta yako ilipofikia; na/au komputa yako ilivyozuiliwa upatikanaji wa huduma. [Port 6667]
  • Mtu mmoja anatumia Tor kupakua filamu ya Vin Diesel, na ISP wako anapata taarifa ya DMCA. Tazama EFF's kiolezo cha majibu ya DMCA ya Tor, ambayo inaelezea kwa nini ISP wako anaweza akadharau taarifa bila dhima yeyote. [Arbitrary ports]

Baadhi ya waendesha huduma ni rafiki kuliko wengine linapokuja suala la Kujitoa kwenye Tor. Kwa kuorodhesha tazama ISP wazuri na wabaya.

Kwa mkusanyiko uliokamilika wa kiolezo cha majibu kwa aina tofauti za malalamiko ya unyanyasaji, tazama mkusanyiko wa violezo. Pia unaweza ukapunguza kiwango tha unyanyasaji unachopata kwa kufuata hatua hizi kwa kutumia exit node pamoja na unyanyasaji mdogo na kupunguza sera za kujitoa.

Pia unaweza kukuta IP zako za Tor relay zimedhhibitiwa upatikanaji kwa baadhi ya tovuti/huduma. Hii inaweza kutokea bila kujali sera zako za kujitoa, kwa sababu baadhi ya makundi hayatambui wala kujali kuwa Tor ina sera za kujitioa. (Kama utakua na anwani ya akiba ambayo haitumiki kwa kazi nyingine, unaweza kutumia relay za Tor katika hilo.) Kwa ujumla, tunashauri usitumie kujiunganisha na mtandao wa nyumbani kwako kutoa Tor relay.