Tunasikikita sana, kwamba umeathirika na programu hasidi. Tor Project haijatengeneza malware hii. Watengenezaji wa malware wanakutafuta upakue Tor Browser labda uwatafute wao bila kujulikana kwa fidia ambayo wanaitaka kutoka kwako.

Kama hii ndo mara yako ya kwanza kutumia Tor Browser, tunaelewa kuwa unaweza kudhani ni watu wabaya ambao tunawawezesha watu wabaya pia.

Lakini zingatia programu yetu hutumika kila siku kwa malengo mengi ya wanaharakati wa haki za binadamu, waandishi wa habari, waathirika wa unyanyasaji wa majumbani, watoa taarifa, maafisa utekelezaji wa sheria, na wengine wengi. Kwa bahati mbaya udhibiti ambao programu yetu unaweza kutoa kwa makundi haya ya watu unaweza pia kutumiwa vibaya na wahalifu na watengenezaji programu hatarishi. Tor Project haisaidii au kusamehe utumiaji wa programu yetu kwa lengo la kuhasidi.