Ikiwa relay yako ni mpya kwa kiwango fulani, basi ipatie muda. Tor inachagua relays inavyoona inafaa kwa kutumia mbinu za utafiti wa kisayansi kulingana na ripoti kutoka kwa Mamlaka za kiwago cha data inayosafirishwa. Mamlaka hizi hufanya vipimo vya uwezo wa relay yako na, kwa muda, huongoza usafirishaji wa data zaidi hapo hadi inapofikia kiwango bora. kipindi cha mzunguko wa relay mpya umeelezwa kwa undani zaidi katika chapisho hili la blogi. kama umekua ukiendesha relay kwa mda na bado una suala linatatiza jaribu kuulizia kwa tor-relay list.