Mashambulizi ya kuzuia upatikanaji wa huduma zilizosambazwa (DDoS) hutegemea na kuwa na kundi la maelfu ya kompyuta ambazo hutuma mfufulizo wa upekuzi kwa mwatirika. Ikiwa lengo ni kuzidisha nguvu za kiwango cha taarifa kwa mwathirika, kwa kawaida hutuma pakiti za UDP kwakua hazihitaji wadau au uratibu.

Lakini Tor husafirisha njia sahihi za TCP tu, sio kila pakiti za IP, huwezi kutuma pakiti za UDP katika Tor. (Huwezi kufanya fomu maalum katika shambulio hili kama mafuriko ya SYN.) Hivyo mashambulizi ya DDoS hayawezekani katika Tor. Tor pia hairuhusu ukuaji wa mashambulizi ya data dhidi ya tovuti za nje: Unatakiwa kutuma byte kwa kila byte ambayo mtandao wa Tor itakakutumia katika sehemu uliyopo. Kwa ujumla, washambuliaji wanaoendesha data za kutosha kuzindua ufanisi wa mashambulizi ya DDoS wanaweza kufanya vizuri bila Tor.