Kwa ujumla ni haiwezekani kutokujulikana kabisa, hata kwa Tor. Ingawa kuna baadhi ya mambo unaweza kufanyia mazoezi ili kuboresha kutokujulikana kwako wakati unatumia Tor na ukiwa nje ya mtandao.

Tumia Tor Browser na programu muhsusi iliyosanidiwa na Tor

Tor haiwezi kulinda muingiliano yote ya mtandao wa intaneti wa kompyuta yako unapoendesha programu hiyo. Tor inalinda programu tu ambazo zimefanyiwa usanidi sahihi wa usafirishaji wa data kupitia Tor.

Kuvinjari tovuti:

Kusambaza faili:

Dhibiti maelezo unayotoa kupitia fomu za tovuti

Ikiwa utatembelea tovuti kwa kutumia Tor Browser, hawatafahamu wewe nani au sehemu yako sahihi ulipo. Japokuwa tovuti nyingi huuliza zaidi juu ya taarifa binafsi kuliko wanavyohitaji kupitia fomu za tovuti. Ikiwa utangia katika tovuti hiyo, bado hawataweza kujua sehemu uliyopo lakini watajua wewe ni nani. Zaidi ya hayo, utatoa: jina, barua pepe, anwani, namba ya simu, au taarifa zingine binafsi, hautakuwa tena mtu usiyejulikana katika tovuti hiyo. Njia nzuri ya kujilinda ni kuwa makini na kuchukua tahadhari kipindi unajaza fomu za tovuti.

Usitumie torrent na Tor

faili kwa njia ya Torrent zimeonekana kupuuza mipangilio ya proksi na kufanya mawasiliano moja kwa moja hata wanapoelekezwa kutumia Tor. Hata kama programu yako ya torrent imeunganishwa kupitia Tor pekee, unaweza kutana mara chache anwani yako halisi ya IP katika ombi la GET ya tracker, kwa sababu ndivyo torrent inafanya kazi. Sio wewe tu Ondoa utambulisho wa usafirishwa wa data ya torrent na mfuatao mwingine wa usafirishwaji wa data wa tovuti ya Tor njia hii, utapunguza kasi ya mtandao mzima wa Tor kwa kila mtumiaji.

Usiwezeshe au kusanikisha browser plugins

Tor Browser itazuia programu ya kivinjari kama vile Flash, RealPlayer, Quicktime na nyinginezo: zinaweza kuendeshwa kuonyesha anwani yako ya IP. Vile vile, hatupendekezi kusanikisha nyongeza ya addons au plugins kwenye Tor Browser, kwani hizi zinaweza kukwepa Tor au vinginevyo kudhuru kutokujulikana kwako na faragha.

Tumia toleo la HTTPS la tovuti

Njia ya Tor itahifadhi data yako kwa kutumia teknolojia ya kusimba, ndani na nje ya mtandao wa Tor, lakini usimbaji wa usafirishaji wa data yako kwenda kwenye tovuti ya mwisho unategemeana na tovuti husika. Ili kusaidia kuhakiki usimbaji wa tovuti, Tor Browser ikiwemo HTTPS-Only Mode kulazimisha kututumia HTTPS iliyosimbwa katika tovuti inayoiunga mkono. Walakini, unaweza kuendelea kuangalia anwani ya URL katika browser ambayo inawezesha tovuti kukupata taarifa nyeti ili kuzionesha padlock au onion icon katika sehemu ya kuandika anwani, ikiwemo https:// katika URL, na kuonesha jina sahihi linalotarajia na tovuti. Pia angalia michoro ya EFF inayoingiliana ikielezea jinsi Tor na HTTPS zinavyohusiana.

Usifungue nyaraka iliyopakuliwa kupitia Tor ukiwa mtandaoni

Tor Browser kitakuonya kabla ya kufungua moja kwa moja hati ambazo zinasimamiwa na programu za nje. USIPUUZE ONYO HILI. Unapaswa kuwa makini wakati unapopakua nyaraka kupitia Tor (hususani DOC na mafaili ya PDF, isipokuwa unapotumia PDF viewer iliyotengenezwa katika Tor Browser) nyaraka hizi zinaweza kukusanya vyanzo vya mtandao ambavyo vitapakuliwa nje ya Tor kwa kutumia programu tumizi inayozifungua. Hii itaonesha anwani yako ya IP isiyo ya Tor. Ikiwa lazima utashughulika mafaili yaliyopakuliwa kupitia Tor tunapendekeza sana ama kutumia kompyuta ambayo haijaunnganisha, au kutumia dangerzone kutengeneza mafaili ya PDF salama ambayo utaweza kuyafungua. Hata hivyo, bila ya kuwa na sababu ya msingi ni salama kuitumia BitTorrent na Tor kwa pamoja.

Tumia bridges na/au tafuta kampuni

Tor inajaribu kuzuia wadukuzi kujifunza ni tovuti zipi umejiunganisha nazo. Walakini, kwa chaguo la msingi, haimzuii mtu anaye kutazama katika usafirishwaji wa data za mtandao kwa kujifunza kwamb unatumia Tor. Ikiwa hii ni muhimu kwako, unaweza kupunguza hatari kwa kusaidi Tor kwa kutumia bridge badala ya kuuunganisha moja kwa moja katika mtandao wa Tor. Mwishoni njia nzuri ya ulinzi ni mbinu ya kijamii: kadri watumiaji wa Tor wavyoongezeka wanakuwa karibu na wewe na maslahi tofauti zaidi yako, hatari inakuwa ndogo ukiwa mmoja wao. Washawishi watu wengine watumie Tor, pia!

Kuwa nadhifu na jifunze zaidi. Elewa nini Tor inafanya na ambacho haikifanyi. Orodha hii ya mitego haijakamilika, na tunahitaji msaada wako kutambua na kuweka kumbukumbu wa mambo yote.