kwa kushea faili kupitia Tor, OnionShare ni chaguo zuri. Onion share ni nyenzo huru kwa ajili ya ulinzi na kutojulikana wakati wa kutuma na kupokea mafaili unapotumia Tor onion services. Inafanya kazi kwa kuanzisha seva ya wavuti moja kwa moja kwenye kompyuta yako na kuitengeneza kama anwani ya wavuti ya Tor isiyoweza kubashiriwa ambayo wengine wanaweza kuitumia kwenye Tor Browser kupakua faili kutoka kwako, au kupakia faili kwako. Haihitaji kuweka seva tofauti, kutumia huduma ya kushirikisha faili ya watumiaji wasio wa moja kwa moja au hata kuingia kwenye akaunti.

Tofauti na huduma kama email, Google Drive, DropBox, WeTransfer, au njia nyingine ambayo watu hutuma mafaili kwa kila mtu, unapoona onion share haujatoa ruhusa ya mafaili ambayo umeyasambaza. Ili mradi unasambaza anwani ya tovuti isiyowezekana kwa njia iliyo salama (kama kunakirisha katika programu ya ujumbe iliyosimbwa) hakuna mtu isipokuwa wewe na mtu uliyesambazia mafaili.

Onion Share imetengenezwa na Micah Lee.

Exit node nyingi zimesanidiwa kuzuia aina fulani za usafirishaji wa mafaili, kama vile BitTorrent. Hususan BitTorrent haifanyi kwa siri kupitia Tor.