Unapo peruzi Onion Service, Tor Browser huonyesha aina tofauti za alama za onion kwenye anwani ya bar ikionyesha ulinzi wa ukurasa wa tovuti wa sasa.

Picha ya onion Onion inamaanisha:

  • Onion Services inatolewa na HTTP, au HTTPS ikiwa na cheti ya CA.
  • Onion Services inatolewa na HTTPS na cheti kilichosainiwa chenyewe.

Picha ya onion ikiwa na mkwaju mwekundu Onion ikiwa na mkwaju mwekundu humaanisha:

  • Onion Service hutolewa na muongozo kutoka kwenye URL isiyo na ulinzi.

Picha ya onion ikiwa na alama ya tahadhari Onion ikiwa na alama ya tahadhari humaanisha:

  • Onion Service hutolewa na HTTPS ikiwa na cheti kilichoisha muda wake.
  • Onion Service inatolewa na HTTPS katika kikoa kisicho sahihi.
  • Onion Service hutolewa na mchanganyiko wa URL isiyo salama.