cryptographic signature / Sahihi ya picha

Sahihi ya picha inathibitisha uhalisia wa ujumbe au faili. Huundwa na mmiliki wa sehemu binafsi wa funguo pacha public key cryptography na huthibitishwa na funguo za umma. Ikiwa utapakua programu kutoka torproject.org, utapata sahihi ya mafaili (.asc). Hizi ni sahihi za PGP hivyo basi unaweza kuthibitisha kuwa faili hilo ulilopakua ni sahihi ambalo ulidhamiria kulipata. Kwa taarifa zaidi, angalia how you can verify signatures.