IP address / Anwani ya IP

Anwani ya utaratibu wa mtandao (Anwani ya IP) ni tarakimu (au mchanganyiko wa namba na herufi katika masuala ya IPv6) iliyotolewa lebo kwa kila kifaa (mf, kompyuta, printa) inayoshiriki katika mtandao wa kompyuta kwa kutumia Utaratibu wa Mtandao kwa mawasiliano. Anwani ya IP ni anwani ya eneo la kifaa, sawa na anwani ya eneo halisi. Tor Browser huficha eneo lako kwa kuifanya ionekane kama traffic yako imekuja kutoka kwa anwani ya IP ambayo sio yako.