New Tor Circuit for this Site / Mzunguko mpya wa Tor kwa mtandao huu

Chaguo hili ni muhimu ikiwa exit unayoitumia haiwezi kujiunganisha katika tovuti unayoihitaji, au haipakii vizuri, Kuichagua itasababisha kurasa inayotumika au window kupakiwa upya kwa Tor circuit mpya. Kurasa zingine zilizofunguliwa na windows kutoka katika tovuti ile ile itatumia circuit mpya vile vile mara tu zinapopakiwa upya. Chaguo hili halifuti taarifa zozote binafsi au inayotengenisha shughuli yako, wala haiathiri miunganisho yako ya sasa kwa tovuti zingine.