Tor imeundwa kutetea haki za binadamu na faragha kwa kuzuia mtu yeyote kudhibiti vitu, hata sisi. Tunachukia kuwa kuna baadhi ya watu ambao hutumia Tor kufanya mambo ya kutisha, lakini hatuwezi kufanya kitu chochote ili tuwaondoe katika hilo bila ya kudhohofisha wanaharakati wa haki za binadamu, unyanyasaji wa manusura, na watu wengine amabao hutumia Tor kwa mambo mazuri. Kama tunataka kuzuia baadhi ya watu kutumia Tor, tutaongeza mlango wa dharula katika programu, ambao utafunguka kwa watumiaji wetu ambao wapo katika hatari ya kushambuliwa na utawala mbaya na wapinzani.