Kama ilivyotajwa hapo juu,mwangalizi anaweza kukutizama wewe na eneo la tovuti au kwenye eneo la kutoka Tor yako ili kuhusisha muda wamsongamano wa kuingia kwenye mtandao wa Tor and pia ikiwa inatoka. Tor haitetei juu ya mtindo huo wa tishio.

Kwa namna ndogo zaidi, zingatia kwamba kama mdhibiti au chombo cha utekelezaji wa sheria wana uwezo wa kupata uchunguzi maalum wa sehemu za mtandao, wanauwezo wa kuthibitisha tuhuma ambazo unaongea mara kwa mara na rafiki yako kwa kuchunguza upekuzi wote wa mwisho na kuhusianisha muda pekee ambao umepekua. Vilevile, hii ni muhimu kuthibitisha kuwa wahusika walio shukiwa kuwasiliana wanafanya hivyo. Katika nchi nyingi, tuhuma ambazo zinahitaji kupata hati zinakuwa na uzito zaidi ya muda wa kuhusisha watakaotoa.

Zaidi ya hayo, kwa sababu Tor hurudia kutumia soketi za muunganiko wa njia nyingi za TCP, inawezekana kujiunga na upekuzi wa kujulikana na kutojulikana kwa kutoka katika node iliyotolewa, hivyo kuwa makini na programu unazotumia katika Tor. Labda kutumia watoa huduma wa Tor tofauti na programu hizi.