Kwa muda mrefu, jumuiya ya Tor imekuwa ikiendesha shughuli nyingi siku hadi siku kwa kutumia mtandao wa IRC unaojulikana kama OFTC. IRC imefanya kazi vizuri na sisi, na jamii yetu katika IRC imekuwa ikibadilika kadri miaka inavyosonga mbele na watu wapya kujiunga na njia mpya kuibuka kwa mahitaji maalum ndani ya shirika.

Bridge yenye namba nne

Jumuiya ya Tor inafungua mazungumzo yake ya kila siku kwa kuunganisha jumuiya yetu ya IRC kwenye mtandao wa Matrix. Kwa watumiaji wa kawaida wa Tor, inamaanisha unaweza wasiliana na sisi kwa kutumia programu tumizi rafiki kama Element. #tor:matrix.org au kituo cha #tor IRC vimeunganishwa: popote utakapochagua kutumia, ujumbe wako utasambazwa kwenye jukwaa zote.

Kujiunga na mazungumzo ya wachangiaji wa Tor katika Matrix, unahitaji kuwa na akaunti ya Matrix, watoa huduma kadhaa wanaweza kukupatia. Mojawapo ya haya ni Matrix.org Foundation, ambayo inaruhusu watu kusajili akaunti bure. Unaweza kusajili akaunti katika app.element.io.

Mara tu ukiwa na akaunti ya Matrix, unaweza jiunga Tor Matrix space ili uperuzi Tor rooms, au ujiunge moja kwa moja katika room #tor:matrix.org user support.

Mtandao wa OFTC IRC

Mbadala, ikiwa unataka kutumia IRC unaweza OFTC's web IRC client:

  1. Fungua OFTC webchat

  2. Jaza nafasi zilizowazi:

    NICKNAME: Chochote unachohitaji, lakini chagua nickname (nick) sawa kila muda tumia IRC kuongea na watu kwenye Tor. Ikiwa nick yake imeshatumiwa, utapokea ujumbe kutoka katika mfumo na unapaswa kuchagua nick nyingine.

    CHANNEL: #tor

  3. Bonyeza kuingia

Hongersa! Sasa upo katika IRC.

Baada ya sekunde chache, utaingiza #tor kiotomatiki, ambayo ni chumba cha mazungumzo cha watengenezaji wa Tor, waendesha relay na wanajumuiya wengine.pia kuna watu aina mbalimbali ya watu katika Tor.

Unaweza kuuliza swali katika sehemu ya kuandikia chini kioo cha mbele, Tafadhari usiombe kuuliza, uliza tu swali lako.

Watu wanaweza kujibu mara moja, au kunaweza tokea ucheleweshaji (baadhi ya watu wamejiorodheshwa katika njia za usambazaji lakini wapo mbali na keyboards zao na wanarekodi shughuli za njia za usambazaji ili kuzisoma baadae).

kama unataka kuwasiliana na mtu maalum, anza maoni yako na jina lao na watapokea taarifa kuwa mtu fulani anajaribu kuwasiliana nao.

OFTC mara nyingi hairuhusu watu kutumia webchat zao na Tor. Kwa sababu hii, na kwa kuwa watu wengi huishia kuipendelea yenyewe hata hivyo, unapaswa pia kuzingatia kutumia IRC client.