HTTPS

Tor inazuia watu wasioshiriki katika mawasiliano kujua tovuti ambazo umetembelea. Hata hivyo, taarifa zinazotumwa bila kusimbwa kwa njia ya mtandao kwa kutumia HTTP kawaida bado zinaweza kuingiliwa na exit relay au mtu yeyote wa uendeshaji anaeangalia usafirishaji wa data kati ya exit relay yako na mwisho wa tovuti. Ikiwa tovuti unayotembelea inatumia HTTPS, basi usafirishaji wa data inayotoka kwenye exit relay itakuwa imesimbwa, na haitakuwa wazi kwa watu wanaojaribu kufuatilia mawasiliano yako.

Mchoro ufuatao unaonyesha taarifa zipi zinaonekana kwa wasikilizaji wa siri ukitumia au usipotumia usimbwaji wa Tor Browser na HTTPS:

  • Bonyeza kitufe cha “Tor” kuona data gani inaonekana kwa waangalizi wakati unatumia Tor. Kitufe kitakua cha kijani kuonesha kuwa Tor ipo inatumika.
  • Bofya kifufe cha “HTTPS” kuona data zipi zinaonekana kwa wafuatiliaji unapokuwa unatumia HTTPS. Kitufe kitabadilika na kuwa kijani kuonesha kuwa kuna HTTPS.
  • Vitufe vyote vikiwa vya kijani, unaona data zinazoonekana kwa wafuatiliaji unapokuwa unatumia vifaa vyote.
  • Vitufe vyote vikiwa vya kijivu, unaona data zinazoonekana kwa wafuatiliaji wakati ambao hutumii kifaa chochote.DATA ZA MUHIMU ZA KUONEKANA
site.com
Tovuti iliyokuwa ikitembelewa.
Mtumiaji / pw
Jina la mtumiaji na nenosiri vilivyotumika kwa ajili ya uhakiki.
data
Data zilizokuwa zikisambazwa.
Eneo
Eneo la mtandao iliyopo kompyuta iliyotumika kutembelea tovuti (anwani ya IP ya wazi).
Tor
Kama Tor ilikuwa ikitumika au haikutumika.