Tunaweka katika dhana ya kuwa wastani wa watumiaji hufanya maombi 10 kila siku. Mtumiaji wa tor aliunganishwa masaa 24 hufanya maombi 15 kwa siku, lakini sio watumiaji wote waliounganishwa masaa 24, hivyo tunachagua wastani wa watumiaji 10. Tunagawanya maombi ya saraka na kuzingatia majibu kama namba ya watumiaji. Njia nyingine ya kuiangalia, ni kwamba tunadhania kuwa kila ombi huwakilisha mtumiaji ambaye yupo mtandaoni kwa masaa kumi ndani ya siku moja, kwa hivyo ni masaa 2 na dakika 24.