Chaguo la kuhesabu katika file la torrc inakuruhusu kubainisha kiasi cha juu cha matumizi ya bytes cha relay kwa muda.

  AccountingStart day week month [day] HH:MM

Hii hubainisha wakati wa kuhesabu unapaswa kujipangilia, Kwa mfano, ili kupangilia jumla ya kiasi cha bytes kilichohifadhiwa kwa wiki (ambayo inapangiliwa upya kila jumatano saa 10:00 asubuhi), unaweza kuitumia:

  AccountingStart week 3 10:00
  AccountingMax 500 GBytes

Hii hubainisha kiasi cha juu cha data cha rilei yako kitakachotumwa kipindi inahesabu, na kiwango cha juu cha data cha rilei yako kitakacho pokea wakati wa kuhesabu. Wakati kipindi cha kuhesabu kinapojipangalia (kutoka AccountingStart), kisha hesabu AccountingMax inajipangilia kuwa 0.

Kwa mfano: Hebu tusema unataka kuruhusu 50 GB za usafirishwaji wa data katika kila upande na kuhesabu kunapaswa kupangiliwa adhuri kila siku:

  AccountingStart day 12:00
  AccountingMax 50 GBytes

Kumbuka kuwa relay yako haiwezi kuamka kikamilifu mwanzoni wa kila kipindi cha kuhesabu. Itaendelea kufuatilia jinsi unavyotumia mgao haraka katika kipindi cha mwisho, na uchague vituo visivyo katika mpangilio katika kipindi kipya cha kuamka. Kwa njia hii tunaepuka kuwa na mamia ya relays yanayofanya kazi kuanzia mwanzo kwa kila mwezi kati ya hizo zinaendelea kuwa hai hadi mwisho.

Ikiwa una kiasi kidogo cha kiwango cha data cha kutoa kulinganisha na kasi ya mtandao wako, tunapendekeza tumia mfumo wa kila siku wa kuhesabu, ili usiishie kutumia mgao wako wote kila mwezi katika siku ya kwanza. Gawanya kiasi chako mwezi kwa 30. Unapaswa pia kuzingatia kikomo cha kiwango ili kueneza manufaa yako ya kasi kwa zaidi ya siku: Ikiwa unataka kutoa X GB katika kila upande, unapaswa kupangalia RelayBandwidthRate yako kwa 20*X KBytes. Kwa mfano, Ikiwa una 50 GB za kutoa kila njia, unapaswa kupangilia RelayBandwidthRate yako kwa 1000 KBytes: kwa njia hii relay yako daima itakuwa na manufaa kwa angalau nusu ya kila siku.

  AccountingStart day 0:00
  AccountingMax 50 GBytes
  RelayBandwidthRate 1000 KBytes
  RelayBandwidthBurst 5000 KBytes # huruhusu utumiaji wa data kwa kiwango cha juu lakini hudumisha matumizi ya wastani