Kama Tor relay yako inatumia kumbukumbu zaidi kuliko ulivyotaka, pata baadhi ya dondoo za kupunguza footprint yake:

  • Ikiwa upo katika Linux, unaweza kukutana na tatizo la kupoteza mgawanyiko wa kumbukumbu katika sehemu tofautitofauti katika utendaji wa glibc's malloc. Hii inamaanisha kwamba, wakati Tor inapoachilia kumbukumbu kurudi kwenye mfumo, vipande vya kumbukumbu huwa vimegawanyika na hivyo ni vigumu kuvitumia tena. Faili la kutunza kumbukumbu la Tor husafiri na utendaji wa OpenBSD's malloc, ambayo haina matatizo mengi ya kuhifadhi kumbukumbu katika sehemu tofauti (lakini inahitajika CPU zaidi). Unaweza kuiambia Tor kutumia huu utendaji wa malloc badala: ./configure --enable-openbsd-malloc.
  • IKama unatumia relay yenye kasi kubwa, inamaanisha umeunganishwa katika TLS nyingi za wazi, kuna uwezekano unapoteza kumbukumbu nyingi katika vifaa vya kuhifadhi data vya ndani vya OpenSSL' (38KB+ kwa kila socket). Tumerekebisha OpenSSL katika release unused buffer memory more aggressively. Kama utasasisha katika OpenSSL 1.0.0 au mpya, kitendo cha kuunda Tor mojakwamoja yenyewe itatambua na kutumia tabia hii.
  • Ikiwa bado huwezi kumudu kumbukumbu za kiwango cha data, kumbuka kupunguza kiwango cha data ambacho relay yako imekitangaza. Kutangaza kiwango kidogo cha usafirishaji wa data inawavutia watumiaji wachache, kwahiyo relay yako haitakuwa sana. Angalia chaguo laMaxAdvertisedBandwidth katika kurasa kuu.

Yote haya yalisemwa, relays ya Tor yenye kasi hutumia kumbukumbu nyingi sana. Si jambo la kawaida kwa exit relay ya haraka kutumia MB 500-1000 ya kumbukumbu.