Unapoboresha rilei yako ya Tor au kuisogeza kwenye kompyuta tofauti, hakikisha kuweka ufunguo za utambulisho sawa (zilizohifadhiwa kwenye keys/ed25519_master_id_secret_key na keys/secret_id_key kwenye DataDirectory yako).

Ikiwa wewe ni mwendeshaji wa kiungo hakikisha pia kuwa umeweka pt_state/. Ina data inayohitajika ili kiungo chako kiendelee kufanya kazi na njia ile ile ya kiungo.

Kwa urahisi,kunakili tu juu ya DataDirectory nzima inapaswa kufanya kazi pia.

Unaweza kutaka kuweka nakala rudufu za funguo hizi za utambulisho, pamoja na pt_state kwa kiungo, ili uweze kurejesha rilei ikiwa kitu kitaenda vibaya.