Tunapendekeza programu za iOSKivinjari cha Onion naOrbot kwa muunganisho salama kwa Tor. Kivinjari cha Onion na Orbot ni vyanzo huru, hutumia uelekezaji wa Tor, na imeundwa na mtu fulani ambaye anafanya kazi karibu na Tor Project. Hatahivyo, Apple huitaji kivinjari katika iOS kutumia kitu kinaitwa Webkit, ambayo huzuia Onion Browser kuwa na ulinzi wa faragha kama uliopo katika Tor Browser.

Jifunze zaidi kuhusu Onion Kivinjari. Pakua Kivinjari cha Onion na Orbot kutoka kwa App Store.