Mullvad imekuwa sehemu ya jumuiya ya Tor kwa miaka mingi sasa. Ni wanachama wa Shallot wa (daraja la juu zaidi la uwanachana) wa Programu ya wanachama wa Tor Project na wamekuwa wanachama waanzilishi wa Programu ya wanachama wa Tor Project.

Kipindi Mullvad alipotukaribia tutengeneze kivinjari kwa pamoja, tulikubaliana nae kwa sababu kuna uwiano mkubwa wa thamani kati ya mashirika yetu mawili katika jitihada za kuimarisha faragha na kutengeneza teknolojia iwe inapatikana eneo kubwa zaidi na kufanya ufuatiliaaji wa watu wengi usiwezekane.