Onion-Location ni HTTP header mpya ambazo tovuti zinaweza kutumia kutangaza onion mwenzao. Ikiwa tovuti unayoitembelea ina tovuti ya onion inayopatikana, taarifa ya pendekezo la zambarau itaonekana katika sehemu ya kuandikia anwani ikisema ".onion available". Ukibofya katika ".onion available",tovuti itatafuta data tena na kukupeleka katika onion zingine. Kwa sasa, Onion-Location inapatikana katika Tor Browser ya kompyuta ya mezani (Windows, macOS na GNU/Linux). Unaweza kujifunza zaidi kuhusu Onion-Location katika Mpangilio wa Tor Browser. Ikiwa wewe ni muendeshaji wa onion service, jifunze jinsi ya kusanidi Onion-Location katika tovuti yako ya onion.